Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Daktari Neema Mduma, mhadhiri kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela, Arusha. Nilipenda kufahamu aliwezaje fikia ngazi ya PhD katika umri mdogo, safari yake ilikuwaje kufika huko, nilipenda kufahamu kuhusu utafiti wake sababu, matokeo na mapendekezo yake.
Nilianza kwa kumuuliza Daktari Neema historia ya elimu yake, mawazo yangu yalikuwa amesoma nje ya nchi na ndio sababu amemaliza PhD katika umri mdogo. Daktari ameniambia kila mtu amempa nchi yake anayodhani amesoma huko, hebu sikiliza toleo hili ujue ukweli halisi. Ila kimsingi Daktari anasema, hakuna linaloshindikana kama umeweka lengo ni lazima ulikamilishe ndio nguzo iliyomfikisha hapo alipo.
Niliendelea na mahojiano yangu na Daktari kwa kutaka kufahamu kuhusu utafiti wake, nilipenda kujua sababu, matokeo na mapendekezo yake. Utafiti wake ulilenga kutatua tatizo la wanafunzi kuacha shule yaani “Student Dropout”.
Daktari anasema ametumia Teknolojia ya Akili Bandia (Artificial Intelligence) ili kuweza kutatua tatizo kabla halijatokea tofauti na kuwasaidia wanafunzi wakati tayari ameacha shule. Ameniambia matokeo yake na muhimu hapa ameangalia characters za wanafunzi , au viashiria vya mwanafunzi kutaka kuacha shule. Ametoa mapendekezo yake ambayo ninadhani ukisikiliza utapata vingi zaidi.
Ukiachilia kazi na mafanikio yake kwa kupata PhD, Daktari ameshirki makongamano mengi ndani na nje nchi kwenye eneo la Machine Learning. Pia mimi nimegundua Daktari Neema ni mwandishi mzuri kweli, amepublish papers kadhaa unaweza kupita pale kwenye Website ya chuo cha Nelson Mandela.
Daktari ni mwanzilishi wa initiative ya #BakiShule, lengo ni kuwapa hamasa wanafunzi wa shule kufikia malengo yao. #Baki shule inawakutanisha wanafunzi na role model kwenye elimu, na kuwapa uelewa kuhusu Machine Learning.
Nimeongea mengi sana na Daktari Neema na kubwa amekuwa akishirikisha fursa mbalimbali hebu mfollow pale Twitter (@nakadori) ili uweze kupata fursa nyingi kutoka kwake.
Nina imani mazungumzo haya yatakusaidia na kukupata hamasa na moyo pale ulipokwana, go out and make that happen, hakuna linaloshindikana kutoka kwa Daktari Neema Mduma. #RoleModelWaWengi