Ebwana mambo vipi bina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast.
Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya computer.
Leo tutazungumza namna ya kuweka vipaumbele kwenye kutengeneza mifumo ya kompyuta. Bila kuweka vipaumbele unaweza tengeneza mfumo usioisha au ambao watu hawata tumia.
Hivi karibuni nimekutana na mambo mawili ambayo yamenisukuma andaa podcast toleo la leo. Kama utakuwa umenifollow kwenye mitandao ya kijamii basi unaweza kuwa umekutana na post nitazozungumza hapa.
Miezi michache iliyopita nilipata bahati pita eneo la Buiko, hapa ninaweza sema ni mpakani kati ya mkoa wa Tanga na Kilimanjaro, nilikutana na jamaa mmoja ambaye ametengeza mashine ya kubebea mizigo hapa mini unaweza sema KIRIKUU. Yeye ni fundi hivyo kwa kumia uzoefu wake na ubunifu ametengeza mashine hii yenye uweza wa kubeba mzigo katika jamii yake kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo.
Nilishudia imebeba mzigo mkubwa wa tofali na unaweza angalia kwenye akaunti yangu ya Instagram kuona uwezo wa mashine hiii.
Hivi karibuni pia nimekutana na nukuu ya Artistotle, “Well begun is Halt Done”. Hapa nimeelewa kwamba ninaweza anza jambo kwa hatua fulani ya ukamilifu wake. Ndio, huhitaji weka kila kitu kiwe tayari mwanzo, unaweza anza katika mazingira magumu japo lengo ni kufika mbali ya hapo ulipoanza.
Niambie unatafari vipi juu ya haya mambo, yawezekana kuna jambo ulipanga anza na wewe uliweka sababu za kukufanya usiendelee kamilisha jambo ulilopanga. Pengine ulisema sina hiki au kile ndio maana sijaweza kamilisha.
Mfano mzuri huenda ukawa ulipanga anza kufanya programming lakini huna kompyuta nzuri, ukasema usibiri mpaka utakapo pata muda, au ukasema sasa nina majukumu mengi ukasema usubiri kidogo majukumu yapungue.
Sasa basi, hapa nilitaka zungumza mambo ya kuzingatia wakati unaanza tengeneza mifumo ya kompyuta. Lakini pia ni vyema uwe tayari kujidhibiti juu ya vishawishi utakavyopata wakati umeanza kazi au hata ukiwa katika ya utekelezaji.
Mara nyingi tunapajadili wazo ambalo tunataka lifanyia kazi liwe mfumo maono yake huwa mazuri na yakupendeza sana. Na mara nyingi ili uweze pata na heshima kwa mteja wako utaongea mambo mbalimbali ya kupamba wazo na namna utakavyolitekeleza, mambo ambayo yatayopelekea mteja apate hamu ya kupata mfumo mapema na kusababisha muda wa mradi kufanyika kwa muda mfupi zaidi.
Nilisema mwanzoni utapaswa jizuia, kuna wakati ukiendelea na kazi teknolojia mpya inaweza kuja na kupelekea kazi kuiona itakuwa rahisi kama utatumia teknolojia hiyo. Vumilia maliza na moja uliokuwa unaijua baadae kwenye matoleo ya mbele utaboresha zaidi kutumia teknolojia hiyo mpya.
Pia muonekano wa mfumo wako ni eneo la kutazama sana, kwa unaweza poteza muda mwingi kama hautafanya maandalizi mazuri. Na hapa nazungumza hatua ambayo mara nyingi huwa tunaipotezea kidogo. Hii ni hatua ya User Interface Design, tunaenda chukua template flani au tunaanza bahatisha wakati tunaendelea na kazi. Unaweka rangi ya njano mara unaona haijakaa vizuri unaweka blue na baadae mteja pia unasema weka nyekundu. Mpango hauyaweka haya yalipaswa fanyanyika mapema kabisa.
Ni vizuri sasa tukazingatia mambo haya ili kutafanya mfumo usiishe na pia ukifanya mpaka hatua flani, shirikisha watumiaji wape waanze tumia utapata mchango mkubwa wa namna ya kuboresha mfumo wako. Nakumbuka WhatsApp ilipoanza tulikuwa hatutumi picha tukawa tunatuma ujumbe tuu, baadae picha tukaanza tumiana ila voice note ilikuwa bado hadi sasa tunaweza piga hata simu za maneno na video pia. Huu ndio ukuaji wa mfumo, kutoka hatua moja mpaka nyingine.
Tazama kwa makini uone unaanza na llpi litafuata lipi, yaweke vizuri kwenye mpango kazi wako kisha fanyia utekelezaji kwa kuhakikisha unafikia malengo ulijiwekea.
Kwa haya muchachee ninaamini kuna jambo ambalo umeweza jifunza hapa, na hii ni moja ya jitahada kuweka hamasa au sensitisation kuona namna ambayo tunaweza tengeneza mifumo ya kompyuta.
Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.