Sign up to save your podcasts
Or
Episode 8
Ebwana mambo vipi jina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast.
Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta.
Leo nitakupa chachu kidogo tuu kuhusu Machine Learning, nimejaribu kufuta maana yake kwa Kiswahili sijapata neno lililo rasmi juu ya Machine Learning. Ni imani yangu tutaelewana tuu hakuna tatizo kabisa, ndio Machine Learning.
Dunia ya leo imejazwa na taarifa nyingi, nyingi sana, na tunazipata kidigitali sasa, taarifa hizi zinaweza kuwa picha, muziki, maneno, video na kadhalika. Nikuambie tuu, hali hii haitegemewi kusimama muda mufupi ujao. Taasisi mbalimbali na makumpuni mengi sasa huendesha shughuli zake kwa njia ya mifumo ya kompyuta. Sasa basi Machine Learning imekuja kuleta suluhu ya kuchakata taarifa hizi kwa niaba yako na kukufahamisha nini unapaswa kufanya.
Kimsingi, binadamu tumekuwa tukichakata taarifa toka enzi, na baadae kupitia mifumo mbalimbali iliyopewa maagizo kuchakata taarifa mfano kwa kuandika formula mbalimbali kama unavyofanya kwenye Microsoft Excel na mifumo mingine ya kufanana na huu. Lakini sasa taarifa zinazokusanywa zimekuwa nyingi kupita uwezo wa binadamu kuzichakata na kuweza kupata maana na tafsiri ya taarifa hizo.
Sasa basi, Machine Learning ni uwezo wa mashine au kompyuta kujifunza kwa kutumia taarifa zilizokusanywa na kuweza kutoa maana na tafsiri (insights) kutoka kwenye taarifa hizo.
Machine Learning iko kila mahali sasa, na wengi tumeona hilo hata kama hujaona basi umetumia tayari bila kujua, kwani mifumo mingi mikubwa sasa nyuma ya pazia wanatumia Machine Learning. Wakati kumtag mtu kupitia Facebook ni mfano dhahiri Machine Learning na huwezi tambua mapendezo ya video za kuangalia kupitia YouTube imewezeshwa na Machine Learning.
Bila shaka, labda mfano mzuri kabisa hapa ni Google. Kila wakati unapotumia Google kutafuta jambo, jua unatumia mfumo ambao unatumia Machine Learning nyuma yake ili kuweza tambua jambo unalotafuta na kuweza landana na maslahi yako binafsi kutokana na mazoea yako kwenye mtandao. Kwa mfano, umekuwa ukitafuta video za Diamond Platnumz kupitia Google. Google wakazutunza taarifa za maulizo yako, ili baadae waweze kuchakata taarifa kupitia Machine Learning ili kukupa majibu yatayoendana na mazoea yako. Hivyo ukija wakati mwingine ukiandika Diamond utaletewa taarifa za mwanamziki Diamond Platnumz na sio Diamond, yaani madini almasi.
Leo, Machine Learning inatumika maeneo mbalimbali, kwenye utambuzi wa picha (Image Recognition), Utambuzi wa Ulaghi mitandao (Fraud Detection), Mifumo ya mapendekezo (Recommendation System) hasa kwenye tovuti za mauzo kupitia mitandao (ecommerce website), pia utambuzi wa maneno na sauti.
Uwezo wa Machine Learning umeonekana kwenye maeneo ya Afya kuwezo utambuzi magonjwa ya kisukari (diabetic retinopathy) na kansa ya ngozi (skin cancer). Bila shaka umejionea kwenye upande wa usafirishaji kupitia magari yanayojipaki (self-parking) na yanayojiendesha (self-driving).
Tupo sehemu nzuri sasa, katika majuma kadhaa yajayo tutaendelea na mada hii ya Machine Learning. Nikiwa bado ninaendelea na majaribio tegemea kufahamu zaidi namna ambayo unaweza anza fahamu vifaa (tools) na kuweza andaa mufumo wako utaoweza kutumia Machine Learning.
Kwa haya machache ninaamini kuna jambo ambalo umeweza jifunza hapa, na hii ni moja ya jitahada kuweka hamasa au sensitisation kwa developers wa ndani kuona namna ambayo tunaweza tengeneza mifumo ya kompyuta.
Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.
5
22 ratings