Ebwana mambo vipi, jina langu ni Yesaya. Ninakukabirisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast.
Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya Kompyuta.
Leo tutazungumza wapi utaanzia tengeneza mifumo ya kompyuta, watu wengi wamekuwa wakiniuliza namna gani wanaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta au lugha gani nijifunze ipi ni bora kuliko nyingine. Na wengine hushangaa mambo ninayopost kwenye mitandao ya kijamii na kuuliza hivyo vinini unaweka, jibu linaweza kuwa rahisi kuwa ni Code. Lakini kwa mtu ambaye hayuko kwenye uwanja wa TEHAMA basi huwa natumia muda kidogo fafanua hili.
Hapa huwa napenda anza na mfano wa kawaida kabisa, ili niweze zungumza na mtu kutoka Italia na tuelewane vizuri nitapenda jifunza lugha yake, vivyo hivyo kwa lugha nyingine. Sasa basi uzuri wa kompyuta inaweza tii maagizo yangu kwa mambo nitayotaka itumaa. Lakini nitawezaje ituma kompyuta? Kuna lugha kadhaa ambazo ninaweza kuzitumia kuwasiliana na kompyuta ili iweze nielewa nachotaka na kuweza tekeleza ombi langu.
Zipo lugha maalumu kwa ajili ya kuwasiliana na kompyuta na si kiingereza wala kiswahili au kichina lah, hapa naongelea Java, Kotlin, Swift, C, C++, na kwa wale wakongwe kidogo basi unafahamu kuhusu Pascal, Fortran na Cobol na nyingine nyingi.
Chochote unachoweza fanya kwenye kompyuta yako, simu au tablet kuna mtu alitumia muda wake kuiambia kompyuta kutekeza hayo inayofanya. Mfano mzuri kabisa, ni pale unapopata wazo ambalo unadhani unaweza liweka katika mfumo wa kompyuta. Tuseme wazo lako ni kuwa na mfumo ya mauzo na upate taarifa za mauzo na manunuzi unayofanya. Basi utatumia moja ya lugha za kompyuta kuanza andika maelekezo ambayo tunaita code. Maelezo hayo ni namna ambayo unataka kompyuta ifanye vile wewe unataka na kitaalaam tunaita requirements.
Kazi hii inahitaji mpango mzuri sana na kuweza tafakari kwa kina namna ambavyo kompyuta itatekeleza maagizo utakayo ipa kwa hatua na utaratibu. Kuna wakati mambo huwa mengi hivyo kama mpango sio mzuri au kwa sababu nyingine unaweza sahau jambo na hivyo mfumo ukianza tumika unakumbuka umeacha jambo fulani.
Na changamoto kubwa ni pale unapokea requirements kutoka kwa mteja wako lakini pale unapoendelea na kazi au unahisi umemaliza, mteja anakumbuka jambo au amefurahishwa na kuanza ongeza mambo mengine zaidi. Hivyo, ni vizuri kuwa na mpango ambao utakusaidia telekeza kazi yako.
Sasa basi, ili kuweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta, weka nia thabiti na jaribu anza tumia lugha moja na tekeleza mradi mmoja ili kuona unaendaje. Tafuta watu wanajua wakushauri na kukusaidia na pale unapota changamoto, pia Google, Google mpaka utapate unachotaka. Zipo course mbalimbali kwenye mtandao zitakazoweza kukusaidia anza tengeneza mifumo ya kompyuta, kama tovuti ya YouTube, Lynda.com, Udemy na nyingine nyingi.
Kitu cha kumalizia hapa ni kuwa, utahitaji jitoa kwani utahitajika kuwa up to date kwa kusoma mambo mapya yanayotokea kila siku kwenye lugha uliyochagua. Na pia kuna wakati utakumbwa na changamoto ambayo solution yake huenda ni nukta tuu na kazi ikawa imekutesa kwa muda hata siku mbili au tatu. Ila usivunjike moja unaweza kufikia malengo yako.
Na kwa taarifa tuu, katika mwaka 2018 ripoti kadhaa zimeripoti huko Marekani Software Developer (Watengeza Mifumo) ndio kazi bora zaidi. Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia kuwepo kwa ajira za namba kubwa katika fani ya TEHAMA serikalini, yaani nafasi hadi 39 katika taasisi moja wote ni TEHAMA kuajiriwa kwa wakati mmoja na nyingine zinaendelea tangazwa. Bado fursa za uwekezaji kwenye TEHAMA, mashindano na makongamano mbalimbali yapo mtaani, kikubwa ni uwezo wako kukabiliana na kupigania fursa hizi, jipange kuwa bora sasa.
Haya yote yanaoyesha kuwa kuna fursa nyingi na uhitaji unaongezeka siku hadi siku. Uwezo tunao katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili, hivyo tusiwe nyuma mpaka tufanyiwe au tungoje watalaam kutoka mbali. Tunaweza na tupo tayari kwa wewe kuanza tengeneza mifumo ya Kompyuta sasa.
Kwa haya machache nina imani kuwa jambo umejifunza hapa, na hii ni moja ya jitahida kuweka hamasa au sensitazation kwa developers wa ndani, kuona namna ambayo tunaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta.
Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.