Ripoti mpya kati ya vizazi imetolewa leo, ikionyesha athari za bajeti ya serikali na mitazamo ya uchumi katika miongo minne ijayo.
Naibu Kamishna wa Polisi wa New South Wales Peter McKenna anasema matukio manne tofauti yanayodaiwa kuwa ya unyanyasaji wa nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita yanaonyesha uzito wa janga hilo nchini Australia. Katika tukio lililo ripotiwa katika eneo la Blue Mountains, mvulana wa miaka mitano alikufa, na ndugu zake wawili na mama yake mwenye umri wa miaka 42 walijeruhiwa vibaya baada ya kupatikana na majeraha ya kudungwa visu ndani ya gari katika eneo la Valley Heights.
Kenya imetetea makampuni ya ndani yanayoagiza mafuta yaliosafishwa chini ya makubaliano ya serikali kwa serikali, siku chache baada Kampala kudai kuwa mpango huo ulikuwa umetekwa na madalali hali iliyopelekea kupanda kwa bei ya mafuta nchini Uganda. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa nishati nchini Kenya, Opiyo Wandayi, kampuni kubwa tatu za mafuta katika nchi za Ghuba zinazouza mafuta yake nchini Kenya, zilichagua kampuni za ndani katika mpango huo na kwamba ikiwa serikali ingesisitiza kuchagua makampuni hayo basi mpango huo ungekufa.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.