SIRI ZA BIBLIA

SIRI ZA BIBLIA: NUHU NA GHARIKA YA MAJI/DUNIA NZIMA WATU 8 TU WALIOPONA


Listen Later

Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao agano thabiti (Eb 11:7).

Kadiri ya Mtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya ubatizo (1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni Kanisa, ambalo kadiri ya Agano Jipya ni la lazima kwa wokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake.

Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la mzeituni unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta.

Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa Yesu ambapo alipakwa Roho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu (Mk 1:9-11; Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa binadamu.

Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu sadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili.

Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika ekaristi, ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu (Math 24:37-41).

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

SIRI ZA BIBLIABy SIRI ZA BIBLIA


More shows like SIRI ZA BIBLIA

View all
2Pac - Life So Hard (DJ LeKido Remix) by DJLeKido

2Pac - Life So Hard (DJ LeKido Remix)

69 Listeners

Rich Auntie Chats by Rich Auntie Ventures

Rich Auntie Chats

0 Listeners