Pengine umewahi kujiuliza ni kitu gani huwatofautisha wale waliofanikiwa katika Nyanja Fulani za maisha na wale ambao hawajafanikiwa. Swali hili sio jepesi kujibu kwasababu hakuna jibu moja kwa watu wote yaani inawezekana alichofanya mtu mmoja aliyefanikiwa kisifanane na alichokifanya mtu mwingine.
Lakini tunafanyaje sasa maana ni lazima tujifunze ili na sisi tulioko huku chini tuweze kupanda na kufika juu si unajua juu kuna nice view?
Sasa Smart Generation wakati wote huwaza kuhusu vijana kama wewe ambao wapo katika harakati za kubadili historia ya maisha yao. Hakuna anayechagua kuzaliwa masikini lakini ikitokea umekufa masikini basi kuna mahali wewe mwenyewe unahusika.
Anyway, hatua moja si ndio huanzisha nyingine? Na hatuwezi kwenda popote kama hatujaanzia hapa tulipo?
Well, you guessed right hata hao watu unawaona kwamba wamefanikiwa kuna hatua walipiga mahali Fulani wakati Fulani, they made a move but it wasn’t just any move it was a Smart Move.
Move hii sasa ndio iliyowatoa pale walipo mpaka hapa walipo leo. Ungetamani na wewe ku’make’ a Smart Move kwenye maisha yako? Basi fuatilia series hii iliyoandaliwa na Smart Generation kwa ajili yako.
Sisi kwetu hizi ni Moves na tunafanya moja baada ya nyingine our First Move is Nikki Wa Pilli. Enjoy kumtazama/kumsikiliza