Twasoma hivi g injili ya Mariko 12:37 "..... Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha"
Msomaji, utakubaliana na mimi kwamba; injili ingekuwa jambo la kufikiri sana ili kuelewa, injili ya Agano Jipya ingekuwa kwa watu wachache tu katika dunia hii. Ingebidi uwe mweledi katika filosofia; ama uende shule ama chuo kikuu kufudishua filosofia ili kupokea injili.
Filosofia hawezi kuhubiri injili kwa maskini ama umati, na maskini hawawezi kufuata maelezo ya filosofia.
Injili kwa upande wake inawaelekezea wote. Inamaana ya kuwa neno halihitaji juhudi ya usomi kulielewa. Bali ni kukubali na kutii. Ni kujipeana kwa Yesu Kristo. Maelekezo ya inji ni kuwa; ikiwa una shida na usumbufu ya kuelewa umuhimu wa injili, usikawiye kwa mabishano. Uking'ang'ana kuelewa umuhimu wa injili, utakufa kabla haujaielewa. Fanya jinsi alivyo fanya Nikodemo. Muendee Kristo jinsi alivyo, msikize na kutii. Hili ni jambo la baraka