Twasoma, " vitu vyote hufanya kazi kwa faida ya wale wampendao Mungu". (warumi 8:28)
Yohana mbatizaji(Mathayo 11:2-6) alijipata katika hali ya maahaka gerezani. - "ni wewe ama Kuna aajaye? " akauliza
Paulo vile vile akamwomba Mungu mwiba umwondokee mara tatu. Mungu akamjibu, neema yangu inakutosha. Katika hali hii ngumu ilimpasa kuendelea kumwamini Bwana Yesu hata kama hakuelewa.
Mungu hapa anatufundisha kwamba hata kwenye mwiba, Ywaweza kutimiza makusudi yake maishani mwetu. Paulo alifunuliwa macho kwa Roho akatamka hivi, 'Naona kwamba wakati mimi ni dhaifu, basi nina nguvu' (2 Wakorintho 12:10)
Ndugu na dada, imani yetu yatuongoza, kwake na kukiri "mimi nime jifunza kuridhika katika hali yoyote niliyo nayo". (Wafilipi 4:11)