TANAPA PODCAST

TANAPA PODCAST EPISODE 13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili


Listen Later

Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Katavi. Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika epsodi ya 13.Eneo: Hifadhi ya Taifa KataviMwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Wageni:1.⁠ ⁠Moses Edward Tende ( Mtemi Sigulu) Chifu wa Kabila la Wagongwe.2.⁠ ⁠Lukas Moses Msaga - Mtoto wa Mtemi Sigulu anayefundishwa kurithi mikoba ya Mtemi Sigulu.⁠3.⁠ ⁠⁠Askari Uhifadhi Daraja la Pili - Kimori Shiwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ikolojia, Hifadhi ya Taifa Katavi. Endelea kutufuatilia kupitia Platifomu za TANAPA Podcast.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

TANAPA PODCASTBy Tanzania National Parks (TANAPA)