Tenda Radio Sehemu ya 5 inazungumzia jinsi ambavyo wazabuni wa Tanzania wamepewa upendeleo maalum kwenye sheria mpya, na jinsi ambavyo wanaweza kupata sehemu ya Bajeti ya Serikali iliyotangazwa bungeni (2024/25).
Ndani, utamsikia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi na kiundani tunazungumza na wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri.