Living Theology

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU


Listen Later

Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama vile Roho alivyowajalia kutamka.(MATENDO 2:4)
Uamsho ni kumwagwa kwa Roho wa MUNGU. Wakati Roho wa Mungu akija kwa nguvu juu ya mtu au idadi ya watu kwa wakati mmoja.
Imani kwamba "Ubatizo wa Roho Mtakatifu  hufanyika kwa kila mtu wakati anazaliwa mara ya pili, yaani anapozaliwa upya. Kwa hivyo sisi sote tumebatizwa kwa Roho - sisi sote tumepokea ubatizo huu", hii ni hatia ya kuzima Roho wa Mungu(1 Wathesalonike 5:19).
Katika sura ya pili ya Matendo ya Mitume, Biblia ime weka wazi swala hili. Lakini wanasema, "Ndio, huo ulikuwa ubatizo wa Roho Mtakatifu. Lakini sote tunaupata sasa, na hatujui inapofanyika; inatutokea wakati tunaamini na kutengenezwa upya. Ni kitendo hicho cha Mungu ambacho kinatuingiza katika Mwili wa Kristo. Kwa hiyo hatupaswi kuiulizia.”
Au hoja imewekwa kwa njia nyingine. Inafundishwa kuwa kile kilichotokea Siku ya Pentekoste kilitokea mara moja na milele, kwamba haiwezi kurudiwa, na kwa hivyo ni makosa kwetu kuomba kwamba Roho Mtakatifu anapaswa kumwagwa. Wanasema, “Mungu, Siku ya Pentekoste, alimwaga Roho Wake juu ya Kanisa. Na Roho Mtakatifu  amekuwa katika Kanisa tangu wakati huo. Kwa hivyo, wanafundisha, "ni  vibaya kuomba kumwagwa kwa Roho wa Mungu." Sio ya kushangaza kwamba aina hiyo ya mahubiri imepata umaarufu, watu wameacha kuombea uamsho, na Kanisa liko vile lilivyo leo.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Living TheologyBy Brendon Naicker

  • 3
  • 3
  • 3
  • 3
  • 3

3

1 ratings