TANAPA PODCAST

UHIFADHI NI JUKUMU LA KILA MMOJA


Listen Later

Episodi hii inakuletea uchambuzi wa kina kuhusu Uhifadhi kwa kuzingatia kuwa Uhifadhi wa wanyamapori ni zoezi la kujitolea kulinda na kuhifadhi maliasili kwa maslahi ya Taifa kwa kizazi hiki ma kijacho.


Sikiliza Episodi ya 15 upate elimu kutoka kwa Mzee Ibrahimu Kasontola kutoka katika kijiji cha Lukoma wilayani Uvinza - Kigoma aliyejitolea kwa hali na mali kuhifadhi msitu katika eneo la makazi yake na kupelekea eneo hilo kuwa makazi ya kudumu ya Sokwemtu sanjari na kupanda migomba ambayo hutumika kama chakula pendwa cha wanyamapori hao ambao mara nyingi utawakuta katika makazi ya mzee huyo.


Mwongoza Kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena.


Wageni

1.⁠ ⁠Ibrahim Kasontola (Mzee anayewahifadhi Sokwemtu hao).

2.⁠ ⁠Mwatano Omary (Mke wa Mzee Ibrahim Kasontola).

3.⁠ ⁠⁠Afisa Uhifadhi Mwandamizi - Lameck Matungwa Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Milima Mahale

Usikose kila Jumatatu kupitia Platform za TANAPA Podcast.

TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

TANAPA PODCASTBy Tanzania National Parks (TANAPA)