Living Theology

UTUKUFU WA MUNGU:SABABU HALISI YA UAMSHO


Listen Later

Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu, basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? KUTOKA 32: 9-11
Unaona wasiwasi wa Musa? Anajali jina-yaani, sifa na utukufu-wa Mungu. Hoja yake ikiwa. "Taifa hili, ni watu Wako." Ana jali heshima na utukufu wa Mungu unaohusika katika hali hii. Baada ya yote, hao ni watu Wake; na amewaleta kutoka Misri katika namna ya ajabu na miujiza. Akawapitisha Bahari ya Shamu.
Je! Atawaacha hapa nyikani? Nini Wamisri watasema? Je! Mataifa mengine yatasema nini? Je! Yeye ameshindwa? Aliwaahidi mambo makubwa. Hawezi kuyafanya? Je! Hawezi kuyatimiza?
Musa anapendekeza kwa Mungu kwamba utukufu Wake mwenyewe, heshima Yake mwenyewe, inahusika katika hali hii yote. Ombi hili utalipata bila mwisho katika Zaburi. Kila Wakati, Sala ya manabii kwa Mungu ni, "kwa ajili ya jina lako mwenyewe,"  Maana ya hii ni kwamba , "Hatuna haki ya kusema, lakini kwa ajili ya heshima yako ya milele ee Mungu ."
Kwa hivyo Musa alikuwa na shauku na wivu juu ya jina na utukufu wa Mungu. Na hapa anamwuliza Mungu, kwa ajili Yake mwenyewe, ebu hifadhi utukufu wa jina lako.
...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Living TheologyBy Brendon Naicker

  • 3
  • 3
  • 3
  • 3
  • 3

3

1 ratings