Sio kila mtu wa kumwambia mawazo/ndoto/malengo yako, kwasababu si kila mtu anaweza kuona kile ambacho wewe unaona.Ni mara ngapi una wazo zuri la Biashara, Podcast, Youtube, na ukimwambia rafiki au mtu wako wa karibu wanalizima kwakukwambia/ kukupa ushauri hasi na kukuonesha kuwa ilo wazo ni ngumu kufanikiwa au hailiwezekani kabisa, kuwa tu mkweli ni mara ngapi hii imekukuta.Mara nyingi right, tena wengine waliokuambia hivyo ni ndugu zako wa karibu kabisa familia na hiyo ndo mbaya zaidi.
Ushawahi kuimagine umefungua biashara unayoipenda na imefanikiwa? Ushaimagine unaendesha gari ya ndoto zako? So hayo ni maono ambayo ukifanyia kazi kwa bidii, utafika huku.Lakini kwanza unapeleka kwa mtu anakushauri, lakini majibu yake yamejaa kukatishwa tamaa na maneno hasi tupu.