Wanamuziki mashuhuri akiwemo Angelique Kidjo ni miongoni mwa wanaoshirikikwenye tamasha la kimitandao la kutetea haki za kijamii na ambalo litachangisha fedha wakati wa maadhimisho ya 75 tangu kubuniwa kwa Umoja wa Mataifa.
Kwanza kabisa tuanze na habari za fasihi ambapo mwandishi maarufu wa vitabu kutoka Nigeria Chimamanda Ngozi Adichie, ambaye kitabu chake cha Half of a Yellow Sun kilishinda tuzo bora zaidi ya utunzi kwa wanawake mwaka 2007 sasa tena ameteuliwa kupokea tuzo ya Mshindi wa Washindi miongoni mwa wanawake.
NFL, Pepsi na Roc Nation wiki hiii wametangaza kuwa mwanamziki mashuhuri The Weekend atakuwa miongoni mwa wasaani watakaoshiriki kwenye fainali ya mpira wa American football maarufu kama Super Bowl , Februari 7 mwaka ujao kwenye uwanja wa michezo wa Raymond James mjini Tampa Florida.
Show hizo zilizofanyikia kwenye mji mkuu wa Khartoum hivi karibubi zilihusisha wanamitindo wa kike pamoja na wa kiume wakitembea kwenye jukwaa moja kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu ambayo taifa hilo lilitawaliwa na Bashir.
Rihanna amerejea tena na video mpya ya Amazon Prime iliopewa jina Savage X Fenty Show Vol 2. Show hiyo ya musimu wa fall mwaka huu imeanza Oktob. Kwenye show hiyo, wanamitindo wa kila aina na tabaka wanaonyesha mavazi ya ndani ya wanawake kwa bei nafuu.