Stori kuhusu mwanariadha wa Angola Andre Mathias, akizungumzia maandalizi yake kuelekea kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka huu, pamoja na tuzo za BET ambazo zilifanyika hivi karibuni.
Maua ya kupendeza kutoka mataifa kama China, Italy na kwengineko yaliwekwa kwenye kaburi lake huku mashabiki waliokuwepo wakitoa heshima zao kwa mwanamuziki huyo wa Pop.
Wiki hii miongoni mwa tunayoangazia kwenye Zulia Jekundu ni maisha ya gwiji wa muziki kutoka Afrika Kusini, marehemu Miriam Makeba, pamoja na baadhi ya wateuliwa wa tuzo za Oscar.
Mwanamuziki kutoka Nigeria na mshindi wa Tunzo za Grammy Burna Boy yuko kwenye orodha ya Jarida la Times akiwa ni miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni kwa mwaka 2024.
Mwanamuziki na mwanasiasa wa Uganda Bobi Wine apepea kwenye jukwaa la kimataifa kutokana na movie yake iliokuwa miongoni mwa zilizoteuliwa kwenye tuzo za Oscar za mwaka huu.