Baada ya mvutano wa kisiasa uliojitokeza mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita huko Zanzibar, sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano.
Lakini je, makubaliano hayo yatafungua ukurasa mpya wa demokrasia, au ni hatua ya kujenga utulivu kuelekea uchaguzi ujao?
Makubaliano hayo yaliyosainiwa Julai 9, 2026 yanajumuisha mapitio ya Katiba, mageuzi ya uchaguzi, maboresho ya mfumo wa sheria, kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma, kuundwa kwa chombo cha kisheria cha kusimamia utekelezaji wa makubaliano pamoja na kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Hafla ya utiaji saini imefanyika Ikulu Zanzibar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na viongozi wa dini, serikali na wadau mbalimbali.
Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki hii leo tunaangazia makubaliano ya kisiasa kati ya CCM na ACT-Wazalendo Zanzibar, matarajio yake, changamoto zake na athari zake kwa mustakabali wa demokrasia visiwani karibu tuwe pamoja hadi tamati.