Dhamana

Dhamana

By Jungu Podcast.Education
Download on the App Store

Dhamana episodes

  • MAWAKILI WARUHUSIWA MAHAKAMA ZA MWANZO.
    Marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya mahakama za mahakimu yanaruhusu mawakili kuwawakilisha wateja wao katika mahakama za mwanzo ambapo awali mawakili walikuwa hawaruhusiwi kuwakilisha wateja wao katika mahakama za mwanzo.
    3 min
  • Mgawanyo wa mali baada ya Talaka.
    MGAWANYO WA MALI BAADA YA TALAKA.
    Mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa jasho la wanandoa wote wawili hugawanywa sawa kwa kila mmoja. Mchango katika kupatikana kwa mali hizo ndio sababu kubwa ambayo huzingatiwa katika kugawa mali za ndoa.
    Mchango katika kupatikana kwa mali za ndoa ni pamoja na kazi za nyumbani ambazo hufanywa na wanawake katika ndoa. kazi hizo hutambuliwa kisheria Kama mchango unaompa haki mwanamke kupata mgao katika mali zilizochumwa pamoja baada ya ndoa kuvunjika.
    Mali zinazogawanywa ni zile zilizopatikana kwa nguvu ya pamoja na si mali binafsi za wanandoa waliotengana. Kuna uwezekano kwa wanandoa kuwa na mali binafsi ambazo haziangukii katika mali za ndoa.
    #ijuesheria
    #sheria
    #sheriatanzania
    #mwanasheria
    #jungulasheria
    #sheriahouse
    3 min
  • Matunzo ya mtoto baada ya Talaka.
    MATUNZO YA WATOTO BAADA YA TALAKA.
    Baada ya ndoa kuvunjwa na mahakama, hutolewa amri ya mahakama kuhusu uangalizi na matunzo ya watoto.
    Haki ya kuishi na watoto hutegemea umri wa mtoto au watoto, uwezo wa kifedha wa kuwatunza na ustawi wa mtoto mwenyewe.
    Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 7 hupaswa kuishi na mama kwaajili ya ustawi wake kama mtoto, lakini ni lazima ionekane wazi kuwa mama ana tabia njema na ustawi wa mtoto hautaathiwa.
    Mtoto mwenye miaka zaidi ya saba anaruhusiwa kuchagua kuishi na baba au mama. Baba atawajibika kutoa matunzo ya kifedha kadri ya uwezo/kipato chake kama mahakama itakavyoona inafaa.
    Endapo mama ana tabia za ulevi uliopindukia, uchangudoa n.k mtoto au watoto wataishi kwa baba kwaajili ya ustawi bora wa watoto.
    #ijuesheria
    #sheria
    #jungulasheria
    3 min
  • Hatua za kufuata wakati wa kuomba talaka.
    Mtu yeyote anayetaka kuomba talaka mahakamani lazima kufuata taratibu zifuatazo;
    Kwanza kabisa kifungu cha 101 kinaeleza kwamba muomba talaka anatakiwa kupeleka malalamiko ya matatizo ya ndoa yake kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la Kamishina wa Ustawi wa Jamii au baraza lingine linalotambuliwa kisheria kama kanisani au BAKWATA.
    Baraza la usuluhishi likishindwa kuwasuluhisha litatoa hati ya kwenda mahakamani. Hati hiyo huandikwa katika fomu maalumu inayoitwa “Fomu Na.3”. Kwa mujibu wa kifungu cha 106(2) madai ya talaka yanatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya miezi sita tangu tarehe baraza la usuluhishi la ndoa lilipotoa hati hiyo. Ni muhimu kufahamu kuwa baraza la usuluhishi la ndoa halina mamlaka ya kutoa talaka au kugawa mali za wanandoa bali kazi yake ni kusuluhisha tu.
    Baada ya hapo muomba talaka anatakiwa kutayarisha madai ya kuvunja ndoa na kuyawasilisha mahakamani akiambatanisha vielelezo vyovyote anavyoona vinaweza kuunga mkono madai yake. Kama shauri linafunguliwa mahakama ya mwanzo, basi mhusika anatakiwa kwenda kwenye hiyo mahakama na atapatiwa fomu maalum ambayo atajaza madai yake.
    6 min
  • Kutokuwa na kazi ni kosa kisheria.
    KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU CHA 176(h).
    Kinasema, "mtu mwenye afya kamili ambaye hajishughulishi katika kazi yoyote ya uzalishaji na hana namna yoyote inayoonekana waziwazi ya kujikimu, atahesabiwa kuwa ni mtu mvivu na mzembe na atapaswa kulipwa faini isiyozidi shilingi mia tano au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja.
    #sheria
    #junguupdates
    2 min
  • Dhamana
    Dhamana ni nini, aina za dhamana, vigezo vya kupata dhamana na makosa yasiyodhaminika.
    11 min

About Dhamana

From the publisher's feed

Dhamana, aina za dhamana, vigezo vya kupata dhamana na makosa yasiyodhaminika.