Karibu kwenye taarifa yetu ya khabari ya leo Ijumapili tarekhe 12 Julai, 2020 kutoka Dawati la Khabari la Oman kwa Kiswahili, Maskati, Oman.
http://moh.gov.om/en/ (Wizara ya Afya) imetangaza kuwa watu wengine 1,318 walioambukizwa virusi vya Korona wamesajiliwa, na hivyo kuifanya idadi ya waliotambuliwa kuwa na maradhi ya Covid19 nchini Oman kufikiya 56,015 wakiwemo 257 waliofariki na 36,098 waliokwisha kupona. Wizara hiyo imesema kuwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, watu 9 wamefariki na watu 843 wamepona maambukizo ya virusi vya korona.
http://moh.gov.om/en/ (Wizara ya Afya) imekanusha khabari kutoka katika mitandao ya kijamii kuja kwa vikundi vya madaktari na msaada kutoka nchi za jirani ili kushughulikia hali ya janga hili. Wizara ya afya imesema imejitayarisha kushughulikia hali zozote zile na ikaongezea kuwa imeongeza uwezo katika mustashfa zote. Imethibitisha imani yake kwa wafanyakazi wa afya wote pamoja na raia na wageni, ambao hawaachi kuchukua juhudi yoyote ile iwapo katika kuwakhudumia wagonjwa.
Mikusanyiko ya siri ilisababisha kuongezeka kwa kesi za Covid19. Wakati serikali ya Oman inajaribu kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, maambukizo yamezidi katika hizi juma za karibuni na kusababisha kuzidisha onyo la khatari. Kuzidi kupanda kwa kesi hizi za Covid19 kumesababishwa na tabia isiokubalika ya baadhi ya watu ambao hawafuati maelekezo ya kuzuia kuenea kwake. Wizara ya Afya imelaumu mikusanyiko ya siri ya jamii ambayo ndiyo sababu ya kuongeza kwa nguvu kwa wagonjwa wa korona. Jumla ya qadhiya zilizokuwa na uhakika katika Omani sasa zimepanda na kufikia 54,697, miongoni mwa hizo 1,083 ni za maambukizo mapya yaliyotangazwa siku ya Ijumamosi. Jumla ya qadhiya zote zilizotajwa na Wizara Ijumamosi na wizara, 786 ni za waomani na 297 ni za wakaazi. Idadi ya vifo sasa ni watu 248 miongoni mwao ni wane waliokufa katika saa 24. Khabari zilizotolewa na wizara zinaonesha watu 60 walilazwa siku ya Ijumamosi, kuifanya idadi ya watu waliolazwa katika mustashfa tafauti kufikia 517, ukijumlisha na 133 ambao wako katika vyumba vya mahtuti. Watu lazima wawajibike ikiwa tunataka kuteremshaidadi za waathirika. Kasema Tabibu Ahmed bin Mohammed Al Saeedi, Waziri wa afya, kuwa ni jambo la kimantiki kufuata taratibu za muongozo kujihifadhi wenyewe. Wakati huohuo hakuacha kuona uwezekano wa kufungua sehemu za biashara kuwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizo, Waziri akasema bado watu wanakutana katika majumba kusherehekea harusi na kuratibu dhifa za karamu za kuzaliwa. Ni lazima tujiwekee nidhamu kuhakikisha tutabakia salama. Hivyo basi, tukitoka nje ni lazima tuvae barkoa za kujikinga na maradhi na tusitoke nje isipokuwa kwa dharura, Waziri alinasihi.
Shirika la Ndege la https://www.omanair.com/en (Oman Air) limetangaza kuwa litafanya Safari tatu za ndege kuelekea Frankfurt, Ujerumani, tarekhe 16, 22 na tarekhe 29 ya mwezi ujao wa Julai. Safari hizo ni maalum kutoka Maskati kwenda Frankfurt na kurudi Maskati. Shirika hilo limetoa raqamu za simu +968 9356 1117 na +968 24765 142 na pia barua-pepe [email protected] kwa ajili ya watuwanaopendelea kuwekeza tadhkira zao, likiwaomba kuwasiliana baiina ya saa mbili asubuhi na saa kumi jioni kwa majira ya Oman, kuanzia Ijumapili hadi Al Khamis.
Oman Kwa Kiswahili inaendelea kukuombeni msiache kuchukuwa khatuwa za kujilinda na kuulinda umma dhidi ya janga la Covid19. Timiza wajibu wako kadiri ya uwezo wako.
Tunakukumbusha kuwa unaweza kupokea taarifa zetu za khabari kupitia https://podcasts.apple.com/us/podcast/id1514101043 (Apple Podcasts), https://podcasts.google.com/feed/aHR0cHM6Ly9mZWVkcy5jYXB0aXZhdGUuZm0vb21hbmt3YWtpc3dhaGlsaS8 (Google Podcasts), https://open.spotify.com/show/1As3nxikY7KJ1MrULrqWpW?si=55ixBuRERmqR6Ye_FDpGwg (Spotify) na vituo vyengine vya Podcasts. Unachotakiwa kufanya ni kupakia Podcasts yoyote kati ya hizo kwenye simu yako ya mkononi na ikisha, kutafuta Oman Kwa Kiswahili na kujisajili kwenye mkondo wetu. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kutusikiliza...