Karibu kwenye episode ya 58 ya KijiweNongwa ambayo pia ni episode yetu ya mwisho kwa mwaka 2023.
Tunazungumzia nyimbo mpya kutoka kwa Whozu, Maua Sama, Stamina na K2ga. Tunaambaa zaidi na kujaribu kuelewa nini kinaendelea kati ya Loui na Label yake ya Legacy Records.
Ipi ni nyimbo ya Mwaka? Tunazungumza kuhusu nyimbo kubwa mwaka huu na kuiteua moja kuwa nyimbo ya Mwaka.
Nini tukitarajie 2024 kutoka kwenye Bongo Fleva? Tunafunga na mjadala huo.
Tupende kushukuru sana kwa kutusikiliza kwa mwaka huu, na kwa pamoja tunakutakia sikukuu za heri za mwisho wa mwaka wewe na wapendwa wako.
Mpaka 2024.
Heri ya Krisimasi🎄 na Mwaka Mpya 🎇