Learn Swahili with SwahiliPod101!
Don't forget to stop by SwahiliPod101.com for more great Swahili Language Learning Resources!
-------Lesson Dialog-------
----Formal ----
Maadhimisho ya Mwaka Mpya Nchini Kenya
Tamasha ya mwaka mpya ni mojawapo ya sherehe ambazo husherehekewa kote ulimwenguni. Sherehe hii huja wiki moja tu baada ya sherehe ya Krismasi. Wakenya hawaachwi nyuma katika kuadhimisha sikukuu hii inayoashiria mwisho wa mwaka mmoja na mwanzo wa mwingine. Huwa ni wakati wa karamu na furaha watu wanapokutana na marafiki na jamaa zao. Watu hujawa na matarajio na kuweka maazimio yao kwa ajili ya mwaka mpya huku wakitumai ya kwamba mwaka mpya utaleta heri njema na fanaka katika maisha yao.Nchini Kenya, siku ya mwaka mpya huwa likizo na kwa hivyo wakati mzuri kwa familia na marafiki kukutana. Pia ni wakati ambapo watu kubadilishana zawadi na pia kutuma arafa za heri njema kwa marafiki na jamii. Wakenya wana njia mbalimbali za kuukaribisha mwaka mpya.Watu wengi hukutana katika makanisa, mijini na pia mashambani ili kumshukuru mungu kwa mwaka ulioisha na kuomba kuwa mwaka mpya uwe wa fanaka. Mwaka mpya hupokewa kwa shangwe na nderemo na baadaye umati husubiri waasi kutoka kwa wakleri. Wakristo husafiri kwa umbali kujiunga na wenzao kuukaribisha mwaka mpya kwa kuwa wanaamini hii ndiyo njia bora zaidi ya kuanza mwaka.Makundi mengine hasa vijana hukusanyika kwa tamasha na kuukaribisha mwaka mpya kwa mtindo. Wasanii mbalimbali hutumbuiza waliohudhuria. Mwaka mpya hukaribishwa kwa nyimbo na densi na vifaa vinavyolipuliwa hewani. Tamasha hizi hupangwa na mandhari ya kupitisha ujumbe fulani kuhusu masuala ambayo yanawaathiri.Wakenya wengine husherehekea kwa kwenda kujivijari katika sehemu mbalimbali za nchi. Nchi ya Kenya ina aina mbalimbali za ndege na wanyama ambao wamehifadhiwa katika mambuga mbalimbali; hivyo wakenya wana chaguo kubwa pa pahali watakakoenda. Kuna pia mwambao ambapo kuna fukwe na ziwa ambako wengi huenda kuogelea.Kuna pia kundi jingine ambalo hukutana katika vilabu kuukaribisha mwaka. Hapa vituko vya aina zote hufanyika , wengine hupanda juu ya magari huku wakipuliza vyombo kama 'vuvuzela' na kupiga kelele za shangwe.Raisi wa jamhuri hii pia hutarajiwa kutoa ujumbe wa mwaka mpya na kuwatakia wakenya mwaka wa fanaka.
----Formal English----
The New Year is the most celebrated festival all over the world. It comes just a week after the Christmas holiday. Kenyans are not left behind in celebrating this great festival, which marks the end of one year and the beginning of another. It is a great moment of feasting and joy as people meet with their friends and relatives. People are always full of expectations as they set their resolutions for the new year and hope that it will bring about good tidings and open a new chapter in people's lives.
In Kenya, the New Year is a holiday and therefore a good time for families and friends to meet for family get—togethers as well as picnics. This is also a time when people exchange gifts and also send messages of goodwill to friends and relatives. Kenyans have diverse ways of ushering in the New Year. Large congregations gather in churches, both in the cities and in the countryside, for a moment to thank God for the year that has ended and pray for good fortunes in the coming year. The New Year is received with jubilation and ululation, and later the clergymen are expected to give a message for the year as they also offer prayers for the congregation. Christians travel long distances to join their fellow Christians in ushering in the New Year, for they believe that this is the best way to begin the year.
Other groups, especially young people, gather for concerts to usher in the New Year in style. Here, entertainment from various artists fills the air. The New Year [...]