Musa akachukua ile hema, akaipiga nje ya marago, mbali na kambi, na kuiita hema ya kukutania. KUTOKA 33: 7
Musa aliiweka hema nje ya kambi - “mbali sana na kambi. ” Sasa hapa kambi ya Israeli wakati huo ilikuwa Kanisa la Mungu. Ndani ya Agano la Kale taifa la Israeli lilikuwa Kanisa katika jangwa. Hili ndilo Kanisa tunalozungumzia. Unaona ni nini Musa alifanya? Alichukua hema hii kutoka katikati ya Kanisa kama ilivyokuwa na kuiweka nje, "mbali sana na kambi." jambo Jipya lisilo la kawaida.
Hakuna uamsho ambao umeshuhudiwa katika historia ndefu ya Kanisa umewahi kuwa harakati rasmi Kanisani. Mara nyingi uongozi rasmi wa Kanisa huenda kinyume na kazi ya uamsho. Kwa hiyo matukio haya huanza nje ya kambi, yaani mbali na uongozi raami wa Kanisa.
Mfano, wakuu wa Matengenezo ya Kiprotestanti, watu kama Wycliffe, Jan Hus, na wengine. Haikuwa rasmi, na maafisa hawakupenda. Ilikuwa vivyo hivyo na Martin Luther.
Hata baada ya matengenezo ya Kanisa la Uingereza, huko kulikuwa na watu ambao walianza kuhisi kuto ridhika. Waliamua kufanya kitu sawa. Ndio asili ya Utakaso. Methodism ilianzishwa na Ndugu wawili Wesley na Whitefield na wengine washiriki wa Kanisa la Uingereza. Lakini hawakuanza kufanya kitu katika Kanisa la England badala yake waliunda kile Klabu yao Takatifu, nje ya kambi.
Hakuna uamsho ambao umewahi kushuhudiwa katika Kanisa uliowahi kutokea rasmi katika Kanisa.