Makala hii imeangazia hali ya usalama inayojiri huko mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako Kundi la waasi wa M23 likiungwa mkono na Rwanda lilifanikiwa kuyateka miji miwili muhimu ya Rutshuru na Kiwanja mashariki ya DRC na kuendelea na mapigano kwenye viunga vya mliji hiyo, huku serikali ya Kinshasa ikichukua uamuzi wa kumfurusha Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku Juhudi za kimataifa zikiendelea kuzipatanisha nchi hizo mbili.
Kuangazia hili tumewaalika profesa Pacifique Malonga, ni mtaalamu wa sias aza Rwanda akiwa jijini Kigali nchini Rwanda naye Guerschom Kahebe ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za DRC akiwa Calfornia nchini Marekani.