Nukta the Podcast

Nukta the Podcast

By Nukta HabariNewsEntertainment News
Download on the App Store

Nukta the Podcast episodes

  • Ukame ulivyowarudisha wafugaji kwenye umaskini Tanzania

    Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini.

    Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni wa mwaka 2021 umemfanya apoteze sehemu kubwa ya mali na kumrudisha kwenye umaskini.

    Tofauti na miaka mingine, mvua hizo zilichelewa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa malisho na maji maeneo mengi wilayani Maswa, kama anavyosimulia Herimina Mkude.

    6 min
  • Mbinu zitakazosaidia kudhibiti taka za baharini

    Kudhibiti uchafuzi wa bahari Serikali na wadau wanasema taasisi za utafiti na viwanda zinahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuimarisha mifumo ya ulejerezaji taka. Pia kupiga marufuku kabisa matumizi ya chupa za plastiki na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira ya bahari kama anavyoripoti Suleman Mwiru. 

    6 min
  • Gharama kubwa zinavyorudisha nyuma jitihada za kuokoa mazingira Wilaya ya Kibaha

    Baada ya kubaini faida na urahisi wa kutumia nishati ya gesi kupikia, mwalimu wa moja ya shule za sekondari wilayani Kibaha aliamua kuchukua hatua.

    Alianza jitihada za kutumia gesi kuongeza ufanisi katika mapishi shuleni kwao na kupunguza kiasi cha kuni zinazotumika kupikia ili kuokoa mazingira. Hata hivyo, changamoto iliyobaki ni gharama kubwa za kupata nishati hiyo. Herimina Mkude anatujuza zaidi.

    6 min
  • Changamoto zinapokuletea fursa

    Ni filamu ya "Fine Wine", inayomuhusu mwanadada Kaima anayepitia changamoto katika mahusiano. Licha ya uzuri na ‘usmati’ alionao binti huyu, mahusiano yake na kijana Tunji ni pasua kichwa kuliko hata majukumu yake ya kazi.

    Maisha ya Kaima yanabadilika siku ambayo wanakubaliana kukutana na Tunji katika mgahawa fulani, lakini kaka huyo anamwambia mpenziwe kuwa amsubiri kwani kuna jambo la ghafla limetokea.

    8 min
  • Chupa za plastiki za vinywaji vya kuongeza nguvu zinavyochocheo uharibifu wa mazingira

    Kuzagaa kwa chupa za plastiki za rangi zinazotumika kuhifadhia vinywaji vya kuongeza nguvu katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam kumeibua changamoto mpya ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

    Licha ya chupa za maji kuokotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejelezaji, chupa za rangi zimekuwa zikiachwa zikizagaa mitaani kwa sababu wenye viwanda hawazihitaji katika shughuli zao. 

    Nini kinafanyika kudhibiti taka hizo? Herimina Mkude anaeleza kwa undani suala hilo.


    7 min
  • Magugu maji yanavyowatesa watumiaji wa Ziwa Victoria

    Kuendelea kuwepo kwa magugu maji katika Ziwa Victoria kumeibua kadhia mbalimbali kwa watumiaji wa ziwa hilo wakiwemo wavuvi na wamiliki wa boti na meli kwa sababu hutanda katika eneo kubwa na kuzuia shughuli zao.

    Wanafanya nini kukabiliana nayo? Msikilize mtangazaji Herimina Mkude ambaye anatoa ufafanuzi zaidi.

    7 min

About Nukta the Podcast

From the publisher's feed

Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.