
Sign up to save your podcasts
Or


Mapema Agosti mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kukamata magunia 131 ya bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi mkoani Morogoro, katika moja ya operesheni kubwa za kutokomeza dawa za kulevya iliyowahi kufanyika nchini.
Katika operesheni hiyo Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo anasema wakulima hao wa bangi hufanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kuchepusha maji pamoja na kukata misitu ili kufanya kilimo cha zao hilo haramu.
Watu 18 walikamatwa katika operesheni hiyo iliyoshika mjadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya mamlaka hiyo kueleza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakifanya kilimo katika mazingira ambayo si rahisi kufikika.
Hili ni miongoni mwa matukio makubwa ya kudhibiti dawa za kulevya ndani ya miaka mitano, jambo linaloashiria kuwa washirika wa dawa hizo hatari kwa afya ya binadamu wanaendelea kuzalisha licha ya jitihada za Serikali na wadau kuzidhibiti.
Mwaka 2021 tani 22.74 za bangi zilikamatwa nchini Tanzania ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2020.
Aidha, takwimu za uhalifu nchini zilizopo katika kitabu cha hali ya uchumi mwaka 2022 kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha mashamba ya bangi yameongezeka takriban mara mbili ndani ya miaka minne kutoka 49 mwaka 2018 hadi kufikia mashamba 87 mwaka 2022.
Huenda wachimbaji wadogo wa madini Tanzania wakaepukana na athari za afya pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwa wataasili matumizi ya bidhaa mpya ya kusafishia madini (Activated carbon) inayozalishwa nchini.
Bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi itachochea uzalishaji wa madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa kwa kuwa itapatikana kwa urahisi jambo litakaloongeza kasi katika shughuli za uchenjuaji huku mazingira na wachimbaji wakwa salama.
Upatikanaji wa bidhaa hiyo mbadala wa zebaki katika shughuli za uchechuaji itakuwa mkombozi kwa wachimbaji pamoja na jamii ambayo inaweza kuathirika kwa kwa kuvuta hewa, kula chakula au maji yaliyo na sumu ya zebaki.
Shirika la Afya Duniani (WHO), linabainisha kuwa athari za kiafya zitokanazo na zebaki ni pamoja na kuharibiwa kwa mifumo ya neva, kuharibiwa kwa mfumo wa upumuaji, mmeng’enyo, mifumo ya kinga, figo, mapafu na wakati mwingine husababisha kifo.
WHO wamesisitiza kuwa sumu hiyo inaweza kusababisha magonjwa katika mfumo wa fahamu ikiwemo kifafa, kupoteza uwezo wa kuona au kusikia, udumavu pamoja na kupoteza kumbukumbu
Mpango Kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki 2020/25 unabainisha kuwa zebaki ni miongoni mwa kemikali hatarishi inayosababisha athari kwa afya ya binadamu na mazingira duniani
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebarikiwa vivutio vingi vya utalii ambavyo sio tu vinapendezesha nchi bali ni chanzo kizuri cha mapato hususani fedha za kigeni ambazo hutumika kwa shughuli za maendeleo.
Tovuti ya runinga ya Tanzania Safari Channel ambayo hutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, inabainisha kuwa Asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwa ajili ya uhifadhi.
Hii inajumuisha hifadhi za Taifa 22, eneo la hifadhi ya Ngorongoro, mapori tengefu, hifadhi za misitu asilia na misitu ya kupandwa, maeneo ya kihistoria pamoja na hifadhi za bahari.
Maeneo yote hayo ndio kitovu kikubwa cha utalii nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa kitabu cha hali ya uchumi kwa mwaka 2022, kinachotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) hifadhi za taifa ni moja kati ya vivutio vilivyotembelewa zaidi na watalii wa ndani na nje ya nchi.
Mwaka 2022 hifadhi hizo zilitembelewa na jumla ya watalii milioni 1.4 kati yao watalii 787,742 walitoka ndani ya nchi na watalii 697,264 kutoka mataifa mengine yaliyopo nje ya nchi.
Huenda wewe ni miongoni mwa watu wanaofahamu kuhusu uwepo wa hifadhi hizi lakini hujui ni ipi inaongoza kwa ukubwa, inapatikana wapi, na gharama za kufika huko.
Makala hii imeorodhesha hifadhi tano ambazo ndio kubwa zaidi nchini Tanzania pamoja na aina ya vivutio utakavyokutana navyo.
Ziwa Victoria ni moja ya maziwa makuu ya Afrika Mashariki. Ni ziwa ambalo lipo kwenye mstari wa ikweta na limezungukwa na nchi tatu zilizopo Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda.
Ziwa hili ni chanzo cha Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,650 na urefu huo unaufanya kuwa mto mrefu zaidi duniani, Ziwa Victoria ndiyo ziwa kubwa zaidi barani Afrika na lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,800 ambapo ni la pili duniani kwa ukubwa likitanguliwa na Ziwa Superior lililopo Amerika ya kaskazini, kwa ukubwa huu nchi za Rwanda na Burundi zinaweza kuwa visiwa ndani ya ziwa hili.
lakini Mwajuma ni nani hasa, nini kilimsukuma kuwekeza katika uvuvi kazi ambayo inatafsiriwa kuwa nya wanaume zaidi, fuatana na Abdulshakur katika makala hii ya dakika saba, natumai utajifunza mengi.
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao.
Abdushakur Mrisho ametuandalia makala yanayoonesha ni kwa namna gani elimu ya saikolojia inavyoweza kuwakomboa watu hawa na kuwafanya wajione kama watu wengine na kuchangamana na wanajamii wengine katika shughuli za kijamii.
Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.
Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.
Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini.
Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na Idara ya Udhibiti Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa hali hiyo ya uhaba mkubwa wa chakula itashudiwa kati ya mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu.
Nini sababu? Herimina Mkude anasimulia zaidi.
‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika.
Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo.
Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika.
Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, muimbaji Nadia, mtangazaji maarufu Afrika Kusini Andile, nyota wa muziki kutoka Nigeria 2baba na wengineo.
Bila kuwasahau Zari na Diamond, ambao tunaweza sema wamesababisha Watanzania wengi kuitazama show hiyo.
From the publisher's feed