Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Julian Alfons Kidungu, Kutoka Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu Mdabulo Jimbo Katoliki Mafinga, swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Ibrahimu alipozaa na kijakazi baada ya kushauriwa na Sara Mkwee alipona hapati Mtoto.
Je, Ibrahimu alifanya makosa?
Kama alifanya makosa mbona katika Bibilia hatuoni kuwa alitubu?
Kama hakutubu mbona wengine husema kuwa Ibrahimu ni Baba wa Imani?
Kama ni Baba wa Imani, ina maana mitara yaani kuwa na wake wengi waliruhusiwa hapo awali?maana Ibrahimu alikuwa na wake wawili
Wengine husema kuwa yule Mtoto wa kijakazi ndio tawi la Waislamu, Je, kuna ukweli wowote?
L'articolo Je, Ibrahimu alifanya makosa na alitubu? proviene da Radio Maria.