Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Caspary Moses Nyihwili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema, mbona Makatekista Wakike wanaongoza ibada mbalimbali Kanisani, wakati Bibilia imekataza Wanawake kuongoza ibada yeyeto ile katika 1Wakorintho 14; 34-35?