– Ilikuwa siku ya Ijumaa Januari 06, 1989 miaka 35 iliyopita ambapo Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Uaskofu na Mtakatifu Papa Yohane Paul II katika Basilika la Mtakatifu Petro – Mjini Vatican, Roma Italia.
– Familia ya Radio Maria Tanzania inaungana na Baba Askofu Ngalalekumtwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa utume wake uliotukuka ndani ya Kanisa na tunakualika umtakie neno la Baraka na matashi mema katika siku yake hii anapotimiza miaka 35 tangu alipowekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Uaskofu.
– Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alizaliwa tarehe 25 Oktoba 1948 katika kijiji cha Banawanu kilichopo Parokia ya Tosamaganga. Wazazi wake ni Joseph Ngalalekumtwa na Mama ni Magdalena Sekutika. Alibatizwa Parokiani Tosamaganga tarehe 15 Novemba 1956 na siku hiyo alipewa Sakramenti Takatifu ya Ekaristi Takatifu & Kipaimara na Mhashamu Attilio Betramino, I.M.C aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa.
– Ikumbukwe pia kuwa Askofu Ngalalekumtwa aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Upadre April 17, 1973 na ameliongoza Jimbo la Iringa tangu mwaka 1992, itakumbukwa kuwa Mhashamu Ngalalekumtwa aliwahi kulitumikia Jimbo Katoliki Sumbawanga kama Askofu Mwandamizi kuanzia mwaka 1989 – 1992.
– Aidha Baba Askofu Ngalalekumtwa amewahi kuliongoza Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) katika nafasi ya Rais wa Baraza kuanzia 2012-2018.
L'articolo HONGERA KWA MIAKA 35 YA UASKOFU – ASKOFU TARCISIUS NGALALEKUMTWA proviene da Radio Maria.