Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Daudi Fungameza kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Katoliki Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema katika Litania ya Bikira Maria huwa tuna maana gani tunaposema Bikira Maria Mnara wa Daudi, Bikira Maria mnara wa pembe, Bikira Maria nyumba ya dhahabu na Bikira Maria Nyota ya asubuhi?