Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama.
Kufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo.