
Sign up to save your podcasts
Or


Licha ya Kifungu 81[1c] cha katiba kusisitiza uwakilishi wa usawa na haki kwa watu wenye ulemavu bado wanawake wenye ulemavu waliojitosa kwenye siasa,wanakumbwa na ubaguzi wa kisiasa kutoka kwa wapinzani wao na hata wafuasi wa wapinzani hao.
Pia kifungu cha katiba cha 27[5] kinaeleza kuwa Mtu hatabaguliwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja dhidi ya mtu mwingine kwa sababu zozote zilizotajwa au kuzingatiwa katika Ibara ya 4.
Wanasiasa hao wenye ulemavu hukejeliwa na kutengwa katika harakati za kisiasa kufuatia maumbile yao,ubaguzi huo unawaathiri wanasiasa hao wenye ulemavu,hatua inayowafanya wenzao kushindwa kuendeleza azima yao ya kuwania viti vya kisiasa.
Mwandishi:Nuru Mwalimu
Licha ya kuwa na ulemavu Wanawake kutoka shirika la Tunaweza Women Living with Disability wamejitosa katika biashara ya kutengeneza siagi ya karanga almaarufu peanut butter walioipa jina la Onja Utamu.
Siagi hio inatengenezwa kutumia njugu pekee ambazo husagwa kwa kutumia mashini.
Tangu serikali ya kaunti ya Kwale kuongeza idadi ya vituo vya afya nyanjani, Idadi ya wanawake wanaoaga dunia kutokana na changamoto za kujifungua kaunti ya kwale imepungua kutoka wanawake 560 Kila mwaka Hadi wanawake 35 Kati wanawake laki 1 wanaojifungua kote nchini.
By:Mwanaharusi Rashid
Jamii nyingi uhusisha ulemavu na laana pamoja na ushirikina,huku wengine wakihusisha ulemavu huo na kasoro zinazotokana kwa mzazi haswa wa kike.Kufuatia madai hayo baadhi ya wanajamii uonekana kuwatenga watoto wanaozaliwa na ulemavu.
Ukweli ni kwamba watu wenye ulemavu wako sawa tu kama wengine wasio walemavu.Katika Makala haya “Ulemavu Wangu” leo tunaangazia dada watatu waliozaliwa na ulemavu,licha ya baadhi ya watu katika jamii kuwatenga,wazazi wao walijizatiti katika kuwalea na kuwasomesha na kwa sasa wote watatu ni wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wenye ulemavu jijini Mombasa chini ya shirika lao la Tunaweza Women With Disability.
Lucy Chesi pamoja na dadazake wawili wote walizaliwa na ulemavu na cha kufurahisha ni kwamba licha ya kupitia unyanyasaji na kukashifiwa kwa sababu ya maumbile yao,walipuuza kashifa hizo na kujitahidi katika maisha.
Lucy anasimulia stori yake.
By:Trezer Odero
Licha ya kuwa na ulemavu Wanawake kutoka shirika la Tunaweza Women Living with Disability wamejitosa katika biashara ya kutengeneza siagi ya karanga almaarufu peanut butter walioipa jina la Onja Utamu.
Siagi hio inatengenezwa kutumia njugu pekee ambazo husagwa kwa kutumia mashini.
By:Silvia Maina
Idadi kubwa ya wanawake na watoto wenye ulemavu wa akili,ulemavu wa kuskia na wale wanaokabiliwa na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii,wengi wa wanaobakwa hutishiwa maisha na husalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria.
Katika eneo la Kisauni ambapo ninakutana na msichana mwenye umri wa miaka 16 na ambaye ana ulemavu wa akili,pia mtoto huyu ana ujauzito wa miezi 7 alioupata baada ya kubakwa tangu mwezi wa tisa mwaka jana.
By:Nuru Mwalimu
Idadi kubwa ya wanawake na watoto wenye ulemavu wa akili,ulemavu wa kuskia na wale wanaokabiliwa na ulemavu wa kuona wanapitia dhulma mbali mbali ikiwemo ubakaji katika jamii,wengi wa wanaobakwa utishiwa maisha na usalia kimya wasijue wapi pa kwenda ili kupiga ripoti angalau wapate haki zao za kisheria.
Katika eneo la Kisauni ambapo ninakutana na msichana mwenye umri wa miaka 16 na ambaye ana ulemavu wa akili,pia mtoto huyu ana ujauzito wa miezi 7 alioupata baada ya kubakwa tangu mwezi wa tisa mwaka jana.
Nuru Mwalimu anasimulia kwa kina.
Mawasiliano ni mchakato wa kuhamisha taarifa kutoka chombo kimoja hadi kingine.
Mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kama mchakato kati ya wahusika wawili una mwelekeo uliokubaliwa.
Lakini kwa jamii ya watu wenye changamoto ya matamshi, utumiaji wa simu hizo za mkononi hasa kwa mazungumzo ni changamoto kwao,kama anayosimulia mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Idadi ya uchafu wa plastiki baharini imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni, Likiwa ni tatizo kubwa linalokabili mazingira duniani.
Jambo ambalo limeathiri sana upatikanaji wa Samaki kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya bahari eneo la pwani, Lakini kikundi cha Gazi Women Magrove Boardwalk kimejitolea kulinda msitu wa mikoko katika eneo hilo la Gazi ili mbali na kulinda mazingira, pia wapate kipato cha kujikidhi kimaisha.
Kama anavyotueleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Mara nyingi watu wanapougua wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari kutokana na uwepo wa dawa madukani.
Bila kujua kwamba dawa hizo zinaweza kumletea mtu madhara makubwa kwenye afya yake ikiwemo kufanya magonjwa kuwa sugu.
Hatua ambayo imepelekea wahudumu wa afya wa nyanjani katika Kijiji cha Ribe eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, kuelimisha wananchi kuhusu taratibu nzuri za utumiaji wa dawa katika Makala yaliyotayarishwa na mhariri wetu Ruth Keah.
From the publisher's feed