
Sign up to save your podcasts
Or


Ile ndoto au yale maono ambayo umekua nayo, ni kweli ni makubwa na pengine yanaonekana hayawezekani, lakini haijalishi ni makubwa kiasi gani Ila kama ni Mungu amekupa hayo maono basi uwe na uhakika kuwa Mungu amekupa uwezo na atakufungulia milango ya kufanya. Kumbuka kuna watu ambao watafanikiwa kwa wewe kuyatekeleza maono au ndoto hiyo, USIIKATIE TAMAA.
Ni mambo mangapi umekua unapanga kuyafanya ili uwe bora na hujayaanza bado? Kitu gani kinakuzuia kuanza?
Hizo sababu zinazokufanya usianze, ni kweli ? Anza leo kufanya yale uliyopanga kuyafanya.
Watu wengi sana tumekua na uelewa kua maneno yana nguvu, lakini wakati huo huo tumekua tunajitamkia maneno ya kujikatisha tamaa kama "huu mtuhani siwezi faulu, huu ugonjwa ndio ulimuua fulani na mimi siwezi pona" katika episode hii tunakumbushana kujitamkia maneno yenye kujenga kwani maneno yana nguvu ya kujenga au kubomoa.
Watu wengi huwa wanajiwekea malengo na mipango ya kuboresha maisha yao ya kila siku. Katika safari hii ya kuboresha maisha, kuna kujikwaa na muda mwingine kuanguka, kinacholeta tofauti kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni kutokukata tamaa pale mtu anavyoanguka, wengine hubaki hapo hapo alipoanguka na wengine huinuka na kusonga mbele. Katika episode hii, tunakumbushana kutokukata tamaa pale unapoanguka, inuka tena na anza upya au endelea ulipoishia ila usibaki pale ulipoanguka.
Je unaona unaweza au huwezi? Unajiona mshindi au kinyume? Je umewahi kujua uhusiano wa maendeleo yako na unavyojiona? Ungana nasi katika episode hii ili tujifunze pamoja na kukua pamoja.
Je unaona unaweza au huwezi? Unajiona mshindi au kinyume?
Je umewahi kujua uhusiano wa maendeleo yako na unavyojiona? Ungana nasi katika episode hii ili tujifunze pamoja na kukua pamoja.
Tunapoanza mwaka mpya, kuna mambo ambayo yanaweza yakakupa nguvu ya kuendelea kwa ushindi au yakawepo mambo ya kukukatisha tamaa na kuona kua mipango yako na ndoto zako ni kubwa na haziwezi kufikiwa. Katika episode hii ya kwanza ya mwaka 2025, wageni wetu wanatushirikisha kwa undani umuhimu na faida za planning, na hii episode itakusaidia kuinuka tena na kuweka mipango na mikakati ili uweze kuwa na mwaka wa ushindi 2025.
Heri ya mwaka mpya wapendwa wetu sikio podcast tribe.
Mwaka wa kuvunja rekodi ili kuwa bora zaidi.
#recordbreakingyear
#2025goals
Inawezekana mipango yako ya mwaka 2024 haijafanikiwa au imefanikiwa kwa asilimia ndogo, mwaka mpya ni nafasi nyingine ya kufanya upya na kurekebisha pale tulipokosea ili tuwe na matokeo bora n kuwa watu bora zaidi.
From the publisher's feed
This is a platform that allows you to be heard and for you to be an ear to others. It is hosted by two young ladies from Tanzania, East Africa. Mainly touching on every topic from comfortable…