Nahreel: Safari ya Maisha iliyoanzia kwenye vidole
Wakati wazazi wake wakimtambua kama Emmanuel Mkono, Dunia inamtambua kama Nahreel wa Navykenzo.
Ndoto ya Maisha ya Nahreel ilianzia kwenye vidole vyake. Baba akimuona kama mpiga kinanda wa Kanisa, lakini baadae yeye akawa mtayarishaji Mkubwa wa muziki.
Utayarishaji wa muziki ni fani, inabidi kutumia nguvu, muda na rasilimali kujifunza. Na yeye aliamia kutumia urahisi ulioletwa na internet kwenye ulimwengu wa sasa kujifunza, akaanzia mbali mpaka akaweza.
Umaarufu wake ukakua kutoka shuleni wakati anasoma alipoanza, mtaani na mpaka baadae akawa anakutana na wasaniii wakubwa.
Kwake mziki umekua burudani, kazi lakini zaidi sana umekua lifestyle yake. Anasema mziki ulimsaidia kufocus, kujifunza zaidi na kuwa zaidi ya watu wengine walivyomuona.
Mara zote aliamini kwenye ubora wa kazi zake, na malengo yake ilikua ni kuzifikisha mbali. Hii ilimfanya kuwa very selective, kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi ili ziweze kufika kwenye viwango alivyotarajia.
Leo Nahreel yuko hapo alipo, kwa safari iliyoanzia kwenye vidole vyake, baadae ikaenda kwenye akili na kusambaa sehemu zingine.