Wanangu podcast

Wanangu podcast

By Goodluck JosephSociety & CultureArts
Download on the App Store

Wanangu podcast episodes

  • Episode 111 | Pesa Haitakuwa na Thamani Ifikapo 2036? Ft. Baraka Kambi.

    Pale mtu tajiri zaidi duniani anaposema kuwa pesa huenda isiwe na thamani yoyote ndani ya miaka kumi ijayo, ni kauli inayozua maswali mengi kuliko majibu. Akiungana na mgeni wake, Mr. Baraka Kambi, Host anajaribu kuchambua maana halisi ya kauli hiyo iliyotolewa na Elon Musk katika mahojiano yake na jarida la The Economist, huku wakitafakari mustakabali wa pesa katika ulimwengu unaoelekea kutawaliwa na Akili Unde (AI) na roboti.

    25 min
  • Episode 110 | Tunafuata Muziki au Tunatafuta Likes?

    Katika episode hii, host anaibua swali: je, kadri tunavyozidi kwenda mbele, mashabiki wanapoteza uhusiano wao wa moja kwa moja na muziki na kuanza kujali zaidi vitu vinavyouzunguka, kama vile ‘likes’ na engagement kwenye majukwaa ya usambazaji wa muziki kama YouTube? Akiendelea kuchunguza sababu zinazoweza kuwa nyuma ya mabadiliko haya, host anarudisha ‘mic’ kwako na kukuuliza: wewe unaonaje kuhusu hili?

    10 min
  • Episode 109 | Malengo Yanavyoweza Kukupoteza

    Katika episode hii, Host anatoka nje ya box na kukuletea wazo linalokwenda kinyume na matarajio ya wengi: kwamba kama unataka kufanikiwa zaidi katika unachokifanya, huenda ukahitaji kuacha kuwa na malengo. Akirejea kwenye kitabu kilichomtambulisha wazo hili, Host anaeleza kwa nini mfumo wa maisha unaotufundisha kuweka malengo unaweza kuwa na mapungufu yake. Lakini hoja hapa si kwamba tusiwe na malengo kabisa, bali ni kutambua kwamba wakati mwingine malengo hututoa kwenye reli.

    17 min
  • Episode 108 | Fikra Sahihi Huja Kwa Lugha Asili

    Fuatilia jinsi mstari mmoja wa Nash Mc unavyoweza kuzalisha maswali mengi na yenye kutafakarisha kuhusu uhusiano na kutegemeana kati ya lugha na fikra. Ni kama hadithi ya nani alianza kati ya yai na kuku, lakini safari hii ikiwa katika uwanja wa lugha na utambuzi. Je, lugha ndiyo huchochea namna tunavyofikiri, au fikra ndizo huunda lugha tunayotumia?

    14 min
  • Episode 107 | A.k.a Mimi by Ngwair (Uchambuzi)

    Katika episode hii, Host anaichambua album ya kwanza ya Ngwair, A.K.A Mimi, na kueleza mambo aliyogundua baada ya kuisikiliza tena akiwa mtu mzima. Wakati album hii ilipotoka, alikuwa bado mdogo na huenda hakuwa na uwezo wa kuielewa kwa kina kama anavyoweza leo. Safari hii, anaisikiliza kwa mtazamo tofauti; akiunganisha “dots” zilizopo baina ya nyimbo, mambo yanayofanya album hii isimame kama kazi moja yenye mshikamano wa dhamira, ujumbe na ubunifu, pamoja na vipengele vingine ambavyo huenda vilimpita wakati huo. Ugunduzi huo unamfanya aeleze kwa nini anaamini A.K.A Mimi ni album yenye uzito, kina na ubora mkubwa kuliko wengi wanavyoweza kudhani.

    26 min
  • Episode 106 | Usiamini Hadithi Moja Tu

    Katika episode hii, tunaangazia tabia ya kuchukua hadithi ya mtu mmoja na kuitumia kama ushahidi wa kuhitimisha jambo kubwa zaidi. Kupitia mifano ya maisha ya kila siku, katika afya, biashara na social media, tunaona jinsi kauli kama “Mimi ninamjua mtu ambaye…” zinavyoweza kutufanya tufanye maamuzi yasiyo sahihi. Episode hii inatukumbusha kwamba stori moja inaweza kuwa ya kweli, lakini isiwe ushahidi wa kutosha kueleza picha nzima, na kwamba tunapaswa kujifunza kutofautisha kati ya hadithi ya mtu binafsi na ushahidi uliotokana na uchunguzi kabla ya kufikia hitimisho.

    12 min
  • Episode 105 | Kampuni Inayouza Rangi Bila Kuuza Rangi!

    Katika Episode hii, tunaangazia historia ya kuvutia ya Pantone, mfumo uliobadilisha namna dunia inavyotambua, kuwasiliana na kutumia rangi. Tutafuatilia jinsi wazo la kuunda mfumo wa kutambua rangi lilivyoanza, namna Pantone ilivyogeuka kutoka kwenye mfumo wa kawaida wa kuchanganua rangi na kuwa sehemu muhimu ya ulimwengu wa ubunifu, mitindo, matangazo na biashara. Karibu!

    11 min
  • Filamu ya Afrika Iliyowahamasisha Jay-Z na Beyoncé

    Je, ni nini kinachofanya filamu iliyotengenezwa Afrika zaidi ya miaka 50 iliyopita iendelee kuzungumziwa, kupongezwa na hata kuwavutia mastaa kama Jay-Z na Beyoncé? Katika episode hii, host anasimulia Touki Bouki, mojawapo ya filamu kubwa na zenye ushawishi kuwahi kutokea Afrika. Tunafuatilia safari ya wahusika Mory na Anta, lakini zaidi ya hapo, tunaangalia kile ambacho filamu hii inakisema kuhusu Afrika, ndoto za kuondoka, utambulisho, mapenzi na tamaa ya maisha bora. Kwa nini Touki Bouki imeendelea kuwa muhimu kwa vizazi tofauti vya Waafrika? Na ilikuwaje filamu hii ya Senegal ikawafikia na kuwavutia Jay-Z na Beyoncé? Karibu!

    22 min
  • Episode 103 | Usichokimaliza Hukaa Akilini

    Katika episode hii, Host anaangazia dhana ya kisaikolojia inayojulikana kama ‘The Zeigarnik Effect’, inayoeleza kwamba binadamu huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukumbuka kazi au mambo ambayo bado hajayakamilisha kuliko yale ambayo tayari ameyamaliza. Kwa nini hali hii hutokea, na inaathirije maisha yetu ya kila siku? Karibu ufuatilie.

    14 min
  • Kupenda Kwangu 'Titles' Kunanigharimu

    Katika episode hii, host anakukaribisha ndani ya mawazo yake na kukuonyesha mchakato halisi anaoupitia kila anapotafuta title ya episode mpya. Ni safari iliyojaa vita ya ndani kati ya kuandika title inayomridhisha yeye kama ‘mbunifu’ na ile inayopewa kipaumbele na mtandao (algorithms) ili kuwafikia watu wengi zaidi. Anaeleza mapenzi yake ya muda mrefu juu ya titles nzuri tangu akiwa mtoto, hadi changamoto za zama za leo ambapo algorithms zinaonekana kuamua kinachofanya title iwe ‘nzuri’. Episode hii inaibua swali muhimu, Je, ubunifu unapaswa kuongozwa na maono ya mbunifu au na algorithm? Karibu katika mazungumzo haya ya ubunifu na mchakato wa kutafuta title nzuri.

    13 min

About Wanangu podcast

From the publisher's feed

This podcast is hosted by Goodluck Joseph, a curious guy who likes to share all the things he finds interesting in the form of a podcast episode. In other words, this podcast is an extension of his…