Tunaangazia faida za kiafya za wanaume kupashwa tohara .Kenya mwaka 2008 ilizindua kampeni ya kuwatahiri kwa khiari wanaume kuanzia umri wa miaka 15 hii ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na msambao wa virusi vya Hiv katika jamii ambazo huwa hawatahiri. Nchini Rwanda pia ambapo raia wengi hawakuunga mkono tohara ,imeanza kupata mwitikio mkubwa wa wanaume kutahiriwa.