
Sign up to save your podcasts
Or


Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito
Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito
Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kutoka mataifa matano ya Afrika yanashinikiza uwekezaji kwenye kubainisha ,kuzuia na kutoa huduma kwa akina mama waja wazito.
Isitoshe ushirika kwa wanaume kwenye maswala ya uzazi ili wanapokuwa wana ufahamu wanaweza kusaidia kwenye mapambano hayo
Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu.
Kurahisisha safari hiyo kituo cha Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi ; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo.
Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi, wana ari mpya kupambana na wanaongeza furaha katika maisha yao kutokana na kupata marafiki ambao wanahimizana namna ya kuushinda ugonjwa wa Saratani.
Chanjo mpya za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB zitakuwa tayari kufikia mwaka 2029
Hadi sasa chanjo 16 zimekuwa zikifanyiwa majaribio na ikiwa zitaidhinishwa zitaokoa maisha ya watu zaidi ya milioni saba kufikia 2050 haswa katika mataifa yanayoendelea.
Kwa miongo kadhaa chanjo ya pekee ambayo imekuwa ikitumika kuzuia TB ni chanjo ya BCG ambayo mtoto anapewa pindi anapozaliwa.
Wanaharakati wanakiri hatua muhimu zimepigwa kupambana na TB ila uwepo wa chanjo itakuwa hatua muhimu katika mapambano hayo.
Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo .
Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo
Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus Kundu mkurugenzi wa mamlaka ya kilimo na chakula nchini Kenya anafafanua.
Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona
Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika ,Africa CDC kimeonya vifo vinavyohusishwa na usugu wa vimelea vinatarajiwa kuvuka milioni 4 mwaka wa 2050
Mashirika ya kikanda yanasisitiza utekelezwaji wa pamoja wa mikakati ya kukabiliana na usugu wa vimelea ikiwemo afya ya mifugo ,matumizi mazuri ya dawa za antibiotics na dawa za kunyunyuzia mimea kwenye sekta ya kilimo.
Watalaam wa afya wanaonya dawa hadi asilimia 70 zinatumika kwa wanyama na nyingi yazo huishia kwenye vyakula kama nyama,maziwa na hatimaye kusababisha usugu wa vimelea kwenye dawa zinazotumika kwa matibabu ya wanadaam
Ebola imekamilisha siku 100 tangu ilipotangazwa na bado bado haijadhibitiwa
Shirika la kimataifa la VillageReach miongoni mwa mashirika yaliyoalikwa na utawala wa Kinshasa kusaidia juhudi za kudhibiti mwambao hatari wa Ebola Bundibugyo linazungumzia kuhusu mapambano hayo.
Baadhi ya changamoto zinazofanya ugumu mapambano hayo ni ukosefu wa uaminifu kati ya wananchi na serikali ,tamaduni na pia taarifa za uongo.
Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko
Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.
Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi.
Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.
Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida
Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.
From the publisher's feed
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

0 Listeners

88 Listeners

23 Listeners

5 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

15 Listeners

2 Listeners

0 Listeners