Kenya inaanza kufanya vibaya katika riadha kutokana na usimamizi duni na kutohudumiwa vyema kwa wanariadha. Ndiyo kauli ya aliyekuwa bingwa wa mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji , Moes Kiptanui. Aidha, anasema kuwa hakuna juhudi za kukuza vipaji vya vijana. Suala la dawa za kututumua misuli pia ni kero; na serikali imekosa kuweka mikakati kubadili hali. Aidha, tumezungumza na Rais wa Shirikisho la Riadha la Kenya, Jenerali Jackson Towei kuhusu sababu za wanariadha wa Kenya kukimbilia mataifa mengine, vilevile umuhimu wa maandalizi ya kutosha. Mbali na hayo wanahabari wetu, Stephen Mukangai na Walter Kinjo wameshiriki gumzo na Tuwei kuhusu Mashindano ya Wanariadha wa Chini ya Miaka 20, uwanjani Kasarani, Nairobi.