Meneja wa Timu ya Kitaifa ya Basketboli, Sylvia Kamau anasema licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakipitia, timu bado ina uwezo wa kuboresha matokeo hata zaidi iwapo watawapata wadhamini.
Akizungumza na mwanahabari wa michezo, Walter Kinjo, Kamau anasema wako tayari kuwakilisha taifa katika mashindano ya kusaka ubingwa barani Afrika.