
Sign up to save your podcasts
Or


Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC.
Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali.
Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto.
Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.
Raia wa mataifa tofauti tofauti ya Afrika ikiwemo Kenya na Uganda huelekea katika mataifa ya kiarabu kutafta ajira Kila mwaka . Changamoto nyingi zikiripotiwa.Kwenye makala haya Florence amezungumza nao wakina dada wanaofanya kazi huko .
Katika makala haya tujahadili dhuluma za kijinsia swala ambalo limekuwa ni donda sugu kwenye familia zetu, na jamii kwa ujumla.
Wakili Latifa Njoki na wakili Elizabeth Njambi wote kutoka nchini Kenya wanafafanua swala la mrundiko wa kesi mahakani zinazohusiana na dhuluma za kijinsia na suluhu.
Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi.
Makundi haya ni yale ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" .
Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika raia wakiwa hai.
Makala haya yamlika hali wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia 800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .
Siku ya wanawake duniani huadimishwa kila kila tarehe nane ya mwezi machi, kuangazia mchango wa mwanamke katika jamii na pia changamoto zinazowakumba wanawake.
Kauli mbiu ya maadimisho ya mwaka huu, nchini Kenya ni uwekeza kwa wanawake ili kufanikisha maendeleo kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Muungano wa wanamziki nchini Kenya (MAAK), unamtaka mwenyekiti wa Shirika la Hakimiliki ya Muziki ya Kenya, Ezekiel Mutua kujiuzulu kutokana na kile wanadai amekuwa akipora peza za wamziki.
Kupitia taarifa muungano huo, unasema Mutua amekuwa akijilimbikizia pesa za wasanii huku wahusika wakiendelea kusalia maskini.
Ili kufahamu zaidi skiza makala haya.
Ni vigumu kwa watu wachache kutumia usafiri wa beskeli hapa Africa lakini Yusufu raia wa Morocco kwake kutali Africa kwa kuendesha beskeli ni kama kazi.
Benson Wakoli aliketi chini na Yusuf, kuthamini safarizake barani Africa na jinsi gani amekuwa akipokelewa na raia wa mataifa mengine.
Kila mwaka Feb 12 dunia huadimisha siku ya wapendanao, raia wengine wakionesha mapenzi kwa wachumba, pamoja na marafiki.
Lakini nini maana ya valentine? kufahamu zaidi skiza makala haya.
Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya.
Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za kiafrica.
Kufahamu zaidi skiza makala haya.
Katika makala haya tunapiga darubini kuangazia haki za raia wa DRC wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi, na baada ya uchaguzi.
Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mapendo Kusudi alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mwandishi wetu Benson Wakoli.
Kufahamu zaidi skiza makala haya.
From the publisher's feed
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala…

2 Listeners

0 Listeners

1 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

1 Listeners