Share Kizazi Kipya Podcast
Share to email
Share to Facebook
Share to X
By kizazikipyapodcast
The podcast currently has 14 episodes available.
Katika Episode hii Stephen Kaaya amegusia kuhusu kuurudisha uwezo wako wa kuamua cha kufanya kwako, hasa pale unapo kuwa katika tukio ambalo ni la ghafla na hukulitaka. Itakua vyema sana ukichukulia matukio kama hayo kuwa ni fursa, fursa ya kurudisha uwezo wako; uwezo wa kuamua cha kufanya. Chukua fursa alafu twenzetu. Kwa mengi zaidi sikiliza Episode nzima pia tembelea instagram account; @kizazikipyapodcast .
Hauitaji kujua kila kinacho endelea ili kuwa na amani ya kufanya maamuzi. Hauto weza kujua story nzima kuhusu mazingira yanayo kuzunguka au mtu, hata kama akikwambia mwenyewe. Fanya kwa uwezo wako kwa kuamini kile ulicho sikia au kuona kuwa siyo story nzima. Amini kuwa unacho fanya ni sahihi, na fanya unavyo jisikia ndani kwa upendo. Kwa mengi zaidi sikiliza episode hii ambapo nimefafanua zaidi. Pia tembelea instagram account; @kizazikipyapodcast website; kizazikipya.online
Karibu kwenye episode nyingine ya Juma Jipya Edition ambapo Stephen Kaaya amejaribu kuku kumbusha kutuliza moyo kwa kukumbuka wewe ni binadamu na kupunguza mwendo. Tunapo hisi kama kuna uzito ndani, kama huwezi kuendelea, unapata hisia nyingi kwa wakati mmoja na unashindwa kuelewa ufanye nini, kama unajisikia kushindwa na kukata tama. Ni sawa, ni sawa kabisa, wewe ni binadamu na changamoto ni sehemu ya kukua, changamoto ni sehemu ya hatua zitazo kusaidia kusonga mbele. Inawezekana kuzitumia vizuri.
Kwenye episode hii ya Juma Jipya Edition ya Kizazi Kipya Podcast Stephen Kaaya amejaribu kuku kumbusha kusimama tena na kuwa wewe kikamilifu, kuusikiliza ule msukumo ulio ndani yako, ule msukumo wa kujikubali na kuusimamia ukweli wako. Simama, uusimamie, hata kama ikikubidi kufanya hivyo peke yako, sawa!! Ikikubidi kutembea peke yako huku ukiamini huo ni ukweli wako na unafanya hivyo kwa upendo ni jambo zuri na la heri kuliko kufuata mkumbo.
Katika episode hii ya Juma Jipya edition Stephen kaaya amejaribu kuku kumbusha kuwa katika kila mipango tuliyo jiwekea ili tuikamilishe mwaka huu wa 2021 ni muhimu kuwa na misingi imara ambayo ni kwanzia sababu ya kufanya ulilopanga au unalo panga sasa, kiasi cha muda na nguvu utazo tumia kwenye jambo hilo, utayari wako juu ya changamoto zake na la muhimu zaidi ni litakusaidia vipi wewe kupiga hatua yaani kuwa bora zaidi, siyo zaidi ya mwingine bali zaidi ya wewe uliye kuwa mwaka jana.
Kwenye episode hii utakua na Stephen Kaaya akikuelezea kuhusu Kizazi Kipya Podcast kwanzia mwanzilishi na mtayarishaji wake, hadithi ya maisha yake kwa ufupi na nini kilimpelekea kuanzisha KKP, pia natakuelezea mambo ambayo yatakuwa yakiongelewa kwenye hii podcast.
Katika Juma Jipya Edition hii ambayo ni kama episode maalum Stephen Kaaya amejaribu kuongelea mambo matano ambayo amejifunza hadi sasa katika mwaka 2020.Mambo hayo ni:-1. Siyo kuhusu unacho sema kuwa ni sahihi bali ni kuhusu unacho fanya. 2. Kasi yangu ni ile inayo niacha nikiwa na amani moyoni 3. Changamoto zinakuja kunionyesha upande mwingine wa jambo. 4. Kadiri unavyo lazimisha ndiyo kitavyo kuangusha zaidi. 5. Kupiga hatua na kuweka mipaka siyo jambo rahisi hasa ukiwa katika mazingira ya awali.
Katika episode hii ya Juma Jipya Edition ya Kizazi Kipya Podcast nimejaribu kukukumbusha kuhusiana na kufanya kwa wengine; kuonyesha upendo, kuhurumia na kusaidia pia. Ila ili tufanye kwa wengine bila kutegemea kurudishiwa ni lazima tuwe nacho sisi kwanza na ni kwa kuanza kujihurumia, kujipenda na kujijali. Hatuwezi kutoa maji kwa mwingine wakati kikombe chetu ni kitupu na hakina kitu.
Tufanye hayo yote huku tukikumbuka kwenda kwa mwendo wetu na kuwa sisi ni binadamu tuna mapungufu.
Kwenye hii episode ya kizazi kipya podcast juma jipya edition, nimejaribu kugusia kuhusiana na kupiga hatua na kusonga mbele katika kujikubali jinsi tulivyo na katika kufanya mambo mengine pia. Tutapo weza kujikubali na kujiona kuwa tupo sawa jinsi tulivyo then tusonge mbele kwa mwendo wetu manake tumeweza kuangalia yale yote tuliyo pitia yawe ya kutisha, kuhuzunisha na kufurahisha kwa upendo na kwamba yamechangia kuwa hapa tulipo leo.
Mtayarishaji ni Stephen Kaaya. Nashukuru kwa kuwa hapa.
The podcast currently has 14 episodes available.