Siha Njema

Kwa nini ni muhimu kuongeza uwekezaji bunifu katika afya ya watoto


Listen Later

Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika  imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu

Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla.

Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi

Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu.

Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu  wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu.

Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo kwa wakati mwingi huwekeza kwenye miradi inayozingatia matakwa yao.

Aidha ili kuhakikisha kuwa huduma za afya kama uchomaji chanjo zinawafikia wanajamii wote ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kuimarisha huduma za wahudumu wa afya wa jamii ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawafikia watoto walengwa baadala ya wazazi kupata ugumu wa kwenda kusaka huduma hizo.

...more
View all episodesView all episodes
Download on the App Store

Siha NjemaBy RFI Kiswahili


More shows like Siha Njema

View all
Jaridun Duniya - RFI by RFI Hausa

Jaridun Duniya - RFI

0 Listeners

Archives d'Afrique by RFI

Archives d'Afrique

85 Listeners

Appels sur l'actualité by RFI

Appels sur l'actualité

22 Listeners

公民论坛 by RFI - 法国国际广播电台

公民论坛

5 Listeners

 by RFI Brasil

1 Listeners

 by RFI Kiswahili

0 Listeners

 by RFI Tiếng Việt

13 Listeners

 by RFI ខេមរភាសា / Khmer

2 Listeners

Marchés du monde by RFI

Marchés du monde

0 Listeners