2 Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.
Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulikana kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na Malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.
Maandiko yana tudhibitishia ya kuwa utauwa ni muujiza ambao ni mkuu. Ni jambo linalo pita fahamu. Utauwa ni kazi ya Kristo kwetu.
Maswala mengi katika maandiko hatuelewi kwa akili zetu. Mfano; swala la Mungu katika utatu, kuzaliwa kwa Kristo kupitia bikra na kadhalika. Hii ndio maana kazi ya Mungu ni miujiza. Tuna ulizwa kupokea na kuamini neno. Kwa Roho wake yeye huwafunulia siri hii walio mwamini.