Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Maisha Ni Kuthubutu Podcast

By Innocent NgaohEducationSelf-Improvement
Download on the App Store

Maisha Ni Kuthubutu Podcast episodes

  • Jinsi Ya KUJITAMBULISHA DM Au Kwenye Text Kwa Mara Ya Kwanza Unapomtafuta Mtu Yoyote.
    Kama wewe ni wale ambao unawatumia watu DM au text za kawaida Kwa Mara ya Kwanza kama vile "Niaje, Mambo, Vipi, Shwari Mkuu, Harakati Ni Vipi Kiongozi, Mrembo mambo n.k"
    Tambua unakosea sana Tena sana hiyo siyo Kujitambulisha badala ni salamu tu.
    Swali linakuja unajua jinsi ya Kujitambulisha mtu akiona DM au text Yako apate kuijibu bila kupuuzia.
    Unahitaji kuzingatia maeneo matano wakati unamuandika Mtu DM Yako;
    1. Jina la mtu unayemtumia ujumbe wako.
    2. Jina lako.
    3. Shughuli Yako.
    4. Hitaji au shida Yako.
    5. Hitimisho.
    Ukizingatia mambo yote hayo DM zako zitajibiwa mpaka ushangae.
    Kwa mfano...
    "Habari kaka Amos Nyanda naitwa Innocent Ngaoh ni Mwandishi wa Vitabu pia ni mtengeneza maudhui ya mtandaoni ya kuelimisha jamii, nilikuwa naomba usaidizi ni wapi nitapata ujuzi wa copywriting Ili niwe Mwandishi mzuri wa Malala na Vitabu. Natanguliza shukurani."
    Mfano wa DM hiyo akiona tu lazima atajibu, Kwa sababu Iko straight to the point.
    Kujitambulisha ni Sanaa.
    Ndiyo maana...
    Una dakika nane za kujua Namna Rahisi ya Kujitambulisha Ili uwe GURU yaani gwiji.
    Chukua hatua Sasa.
    9 min
  • Jinsi Ya Kuamini UWEZO Wako Na Kuamini Katika Wewe...!
    Umekosa sapoti au kushikwa mkono Katika kazi zako au mapambano Yako?
    Unapitia hali ya kukataliwa na kuona hakuna anayejua thamani Yako Wala Kuamini Katika Wewe?
    Unapitia hali ya kukata tamaa kwenye kitu unachofanya kwa kuwa matokeo yamechelewa.
    Unatamani kuwa Bora ila hujui ufanye Nini?
    Kuna watu wanakurudisha nyuma na kutoamini katika mapambano Yako ila unashindwa kuwaondoa kwa sababu yoyote Ile.
    Basi...
    Episode hii itakupa nguvu na maarifa sahihi ya kuonyesha Uwezo Wako na Kuamini Katika Wewe yaani "BELIEVE IN YOURSELF."
    Sikiliza na ujifunze
    11 min
  • Jinsi Ya Kuacha Tabia Ya Kuwasema Watu Wengine Vibaya...!
    Umekuwa na tabia ya kuwasema watu wengine kwa namna yoyote kwenye maisha yao?
    Hii ni tabia mbaya, lakini hujui ufanye nini ili uache tabia hii ya kimaskini na ni tabia mbaya.
    Inawezekana siyo wewe ila kuna watu wa karibu yako wana tabia hii, basi kupitia maarifa haya utaweza kuwa chachu ya kubadilika kwake.
    Huwezi kumbadilisha mtu ila unaweza kuwa sababu ya yeye kubadilika kama atakuwa tayari kubadilika.
    Kwahiyo...
    Unahitaji sana kuacha tabia ya kuwasema watu wengine vibaya kwa namna yoyote.
    Kwa sababu ni tabia ambavyo inafanya upoteze uaminifu na kuonekana ni mtu wa hovyo.
    Hata kuharibu mahusiano yako na watu karibu yako, hasa pale wakigundua ni tabia yako kuwasema vibaya kwa watu wengine.
    Unahitaji sana kuwa muungwana kwa kutowasema watu wengine vibaya kwa namna yoyote ile.
    Kwa kuacha tabia ya kuwahukumu watu wengine kwa sababu yoyote ile.
    Kupitia episode hii...
    Utajua ni kwa namna gani unaweza kuacha tabia ya kuwasema watu wengine vibaya.
    Baada ya kusikiliza kuwa na uhakika hautakuwa mama ulivyokuwa mwanzo.
    Muda ndiyo sasa wa mabadiliko.
    10 min
  • Uchambuzi Wa Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE? (Nani Kahamisha Jibini Yangu?)
    Nani kahamisha jibini yangu? Ni kitabu ambacho kinakusaidia kukabaliana na mabadiliko ambayo hukutarajia wala kutegemea kwenye kazi na maisha.
    Kitabu kipo kwa mfumo wa stori ambao inahusisha wahusika wanne ambao ni
    1. Sniff
    2. Scurry
    3. Hem
    4. Hew
    Ni kitabu ambacho utajifunza namna ya kukabiliana na mabadiliko kwenye maisha.
    Naamini kupitia uchambuzi wa kitabu hiki utafurahia Sana.
    28 min
  • Jinsi Ya Kuachilia Vitu Na Watu Ambao Wamekuumiza Na Hawatambui Thamani Yako...!
    Kuachilia haijawahi kuwa jambo rahisi hasa kwa watu ambao umewathamani na kuamini wangekuwa na wewe maisha yako yote, lakini ghafla wanakuachia maumivu na kukuumiza kiakili, kimwili, kihisia.
    Inaumiza kuona hawatambui thamani yako na unashindwa kuachikilia na kuishia kuwa na roho ya kutaka kulipa kisasi, uchungu, hasira, msongo wa mawazo na kujichukia.
    Lakini...
    Kupitia episode hii utaweza kuachilia na kwa kujua nini ufanye ili uweze kuachilia na kuishi maisha ya furaha na amani ya moyo.
    Jifunze kuachilia.
    14 min

About Maisha Ni Kuthubutu Podcast

From the publisher's feed

Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha.