Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Maisha Ni Kuthubutu Podcast

By Innocent NgaohEducationSelf-Improvement
Download on the App Store

Maisha Ni Kuthubutu Podcast episodes

  • Sababu 05 Zinazofanya Watu Wakudharau...!
    Hakuna kitu kinaumiza kama watu kukudharau na kubeza uwepo wako si ndiyo?
    Dharau ina maana kwamba wanachukulia poa jambo au kitu fulani pasipo kukipa thamani inayostahili.
    Hivi unajua kwanini watu wanakudharau?
    Ukweli ni kwamba huwezi kuwa mwema na mzuri kwa kila mtu ila inakuwa inaumiza zaidi pale watu ambao umewapa nafasi kubwa kwenye maisha yako halafu wanakudharau.
    Inaumiza sana si ndiyo? Kuna baadhi ya sababu ambazo zinafanya watu wakudharau na ukiweza ku-deal nazo basi dharau zitatoweka na wataanza kukuthamani;
    1. Furaha yako isiwategemee wao,
    Wanakudharau kwa sababu wanajua unawategemea wao ili uwe na furaha kwenye maisha yako, Anza sasa kujipa furaha wewe mwenyewe pasipo kuwategemea wao.
    2. Umeruhusu watu kukuzoea kupita kiasi,
    Thamani ya kitu inakuwa kubwa kikiwa hakipatikani kirahisi, ishi nao vizuri ila weka mipaka ya kutoruhusu mazoea kupita kiasi “Mazoea yakizidi yanaleta dharau”- Lolo Facts.
    3. Kuwa bize na maisha yako,
    Waingereza wanasema “Mind your own business” Kwahiyo acha kufuatilia maisha ya watu na kuwasema vibaya wakijua hilo watakudharau na kukuona ni mtu wa hovyo. Fanya yanayohusu muungwana.
    4. ..............
    5. ..............
    Hivyo basi...
    Mambo matano haya na uhakika yatakusaidia watu wasikudharau, kwa sababu unakuwa umejua nini ufanye ili uongeze thamani yako.
    Kujua mambo yote kwa urahisi na upana ni sehemu moja pekee ambayo ni MAISHA NI KUTHUBUTU PODCAST.
    Kwa sababu utaenda kujua kila kitu kwenye episode ambayo ina madini ya kuongeza thamani yako.
    Cha kufanya ni rahisi...
    Bofya link kwa bio kwa sasahivi Kusikiliza ujue sababu zinazofanya watu kudharau
    14 min
  • Aina 10 Za Ujuzi Ambazo Zitakuingizia PESA (High Income Skills)...!
    Unataka kuingiza pesa na kujikwamua kiuchumi? Kama jibu lako ni ndiyo, basi episode hii inakufaa kwa sababu utaenda kujua aina 10 za Ujuzi ambazo zitakuingizia pesa ni wewe kuchagua Ujuzi mmoja au miwili kisha weka nguvu hapo baada ya mwaka mmoja hadi mitano utaona unaingiza pesa ni uthubutu wako tu. Sikiliza kwa umakini sana
    17 min
  • Ijue Nguvu Ya Mchakato..!
    Ukijua nguvu ya mchakato kwenye maisha yako utapata kuelewa upata kuhusu mafanikio, maendeleo, ukuaji, mabadiliko na kila kitu kinahitaji mchakato. Unataka kujua mchakato haupukeki ni lazima mchakato upitie. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue nguvu ya mchakato.
    10 min
  • Jinsi Ya Kuonyesha Kipaji Chako Hadi Kukupa Matokeo Makubwa...!
    Hivi unakijua kipaji chako au kikubwa ni uhai?
    Pasipo kujali unajua au hujui kipaji chako ila tambua una zawadi ya kipaji ambayo ulipewa na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwako.
    Kwahiyo...
    Kuzaliwa kwako Ina maana una kipaji ndani yako.
    Swali la kujiuliza.
    Je, unakijua kipaji chako?
    Hongera kwa kujua kipaji chako cha .... (Taja kimoyomoyo) Ina maana tayari umeshajua kusudi la kuzaliwa kwako.
    KIPAJI = KUSUDI.
    Lakini...
    Kujua kipaji chako haitoshi ni lazima uonyeshe kipaji chako kwa ulimwengu yaani dunia itambue na kunufaika na kipaji chako.
    Kwa sababu...
    Kipaji siyo kwa ajili yako bali ni kwajili ya kuwatumikia wengine.
    Unajiuliza ni kwa namna gani si ndiyo?
    Ni hivi...
    Milliard Ayo ana Kipaji cha utangazaji ila wananifaika na kipaji chake ni wasikilizaji wake si ndiyo eeh!
    Samatta ana kipaji cha kucheza mpira ila wanufaika ni mashabiki na wapenzi wa mpira wa kufunga magoli na namna anavyochezea mpira.
    Masoud Kipanya ana kipaji cha kuchora ila wanunuifa na michoro ni watazamaji wa michoro yake si ndiyo eeh!
    Joel Nanauka ni mwandishi wa vitabu ila wanuafaika na uandishi wa vitabu vyake ni wasomaji wa vitabu vyake.
    Kuna mifano mingi kuhusu watu wenye vipaji ambao walithubutu kuonyesha vipaji vyako, ni wewe Kuthubutu sasa kuonyesha kipaji chako.
    Kwahiyo...
    Kadiri unavyoonyesha kipaji chako ndivyo unaongeza nafasi ya kufanikiwa kupitia kipaji chako.
    Kumbuka Mafanikio ya kipaji chako si tukio la usiku mmoja ni mchakato.
    Je, unaanza lini kuonyesha kipaji chako kwenye ulimwengu?
    Usiogope kuonyesha Kipaji chako.
    Mwisho kabisa...
    Ni vema ukajua faida za kuonyesha kipaji chako kwa wewe kuniambia hapa chini comment ili tujifunze kwa pamoja.
    Kauli Mbiu: “Maisha Ni Kuthubutu”
    13 min

About Maisha Ni Kuthubutu Podcast

From the publisher's feed

Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha.