Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Maisha Ni Kuthubutu Podcast

By Innocent NgaohEducationSelf-Improvement
Download on the App Store

Maisha Ni Kuthubutu Podcast episodes

  • Jinsi Ya Kuacha Tabia ya Kujilinganisha Na Watu Wengine....!
    Hivi kuna faida yeyote unapata kwa Kujilinganisha Na kutaka kuwa kama watu wengine jinsi walivyo kwenye maisha yako?
    Kwa sababu...
    Kujilinganisha ndio sababu ya kupoteza furaha, kukosa amani ya moyo, kuona umechelewa na Hakuna cha maana umefanya.
    Kumbuka kuwa...
    Ukitaka kuishi maisha ya mtu mwingine kwenye maisha yako, Je maisha yako atayaishi nani?
    Umeshapata jibu si ndiyo?
    Kuna sababu nyingi za kwanini una tabia ya kulinganisha na watu wengine:
    1. Wana ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii,
    2. Kuvaa nguo nzuri na kutumia “Luxury things”,
    3. Wana mafanikio makubwa kukuzidi,
    4. Wana kibali cha kukubalika zaidi kuliko wewe kwenye kitu unachofanya.
    5. Maarifa na hekima kubwa kukuzidi n.k
    Ni baadhi ya sababu nyingi ambazo zinafanya uwe muhanga wa Kujilinganisha Na Watu wengine.
    Ndiyo maana leo...
    Unaenda kujua nini ufanye ili usiwe mtu wa Kujilinganisha Na Watu kwa kujua mambo matano yenye nguvu kuliko kawaida.
    Utajua kila kitu ambacho kitakuwa daraja la wewe kuishi maisha yako halisi bila ya kujifananisha wala kuchanganyikiwa na mambo ya watu wengine.
    Kwahiyo...
    Ni wewe Kusikiliza episode hii kwa kubofya link hapa chini sasahivi.
    14 min
  • Mambo 05 Ya Kufanya Ili Uwe Na Matumizi Mazuri Ya Muda Wako...!
    Tuna masaa 24 ambayo yanatutofautisha kati ya mtu mmoja na mwingine kwa namna ambavyo tunatumia muda.
    Huna muda wa kupoteza kwa kufanya mambo yasiyo Muhimu na msingi kwako na kuacha kufanya mambo ya msingi na Muhimu kwenye maisha yako.
    Kwani hujui muda ukienda umeenda na hauna mbadala?
    Kwani hujui future yako inajengwa na nini unafanya kwenye dakika tano zijazo?
    Kwani hujui wewe ndiyo unapaswa kutumia masaa 24 vizuri Ili upige hatua kwenye maisha yako?
    Ndio maana unahitaji kuwa na nidhamu ya muda ila unajua faida ya Kutumia muda wako vizuri, lakini unapuuzia si ndiyo?
    Lakini...
    Leo utajua mambo matano ambayo ukizingatia basi utakuwa na Matumizi Mazuri ya muda wako;
    1. Tambua vitu au mambo gani yanakupotezea muda,
    Je, ni simu yako inakupotezea muda? Kutazama televisheni muda mwingi? Kucheza ps? Kuzurura? Kumwagilia moyo na Marafiki kila siku? Matumizi makubwa ya mitandao? N.k njia ya kwanza ya kutatua tatizo ni kujua kisababishi cha wewe kupotezea muda wako. Je nini kinakupotezea muda wako?
    2. Anza kuweka vipaumbele,
    Hatupangi kushindwa ila tunashindwa kupanga kwa maana hiyo unapoteza muda kwenye mambo yasiyo ya Muhimu kwako kwa kutokuwa na vipaumbele. Je unajua kazi za umuhimu, Uharaka na zenye matokeo makubwa ni muda gani zinapaswa kufanywa?
    Basi...
    Mambo mengine matatu yaliyobaki jumulisha bonus yatakuwa mambo Manne utapata sehemu moja pekee ambayo ni “Maish ni Kuthubutu Podcast”
    Una sekunde 20 tu za wewe kubofya link hapa chini na Kusikiliza madini haya ya nguvu Ili Uwe Na Matumizi sahihi ya muda wako.
    14 min
  • Aina Tano (05) Ya Marafiki Ambao Hupaswi Kuwapoteza...!
    Hivi unajua kuna Marafiki ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kubwa maishani pia kuna aina ya Marafiki ukiwa nao ni mwanzo wa kukaribisha majanga.
    Unajua kwamba...
    Wewe ni wastani wa Marafiki sita ambao unashinda nao muda mwingi.
    Hata kama hupendi au hauna marafiki, lakini bado unahitaji watu si ndiyo?
    Na watu hawa wakiwa na sifa fulani fulani ni Muhimu kuwatunza maana tupo zama tumezungukwa na Marafiki au watu ambao ni wanafiki sana...
    ...kuna aina tano za Marafiki ambao ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kutoka wa Mungu maana ni Adimu zaidi ya Dhahabu kwenye machimbo ya Chunya pale Mbeya.
    Ha!Ha!Ha! Unacheka au sio.
    Hivi...
    Ukiwa na rafiki ambaye anakuambia ukweli ambao unakujenga unajisikiaje? Jibu unalo.
    Je, Ukiwa na rafiki ambaye anakupongeza unapofanya vizuri unajisikiaje? Jibu unalo.
    Je, ukiwa na rafiki ambaye ni balozi wa kutangaza mazuri na kukunganisha kwenye Fursa na connection za faida?.
    Majibu ya maswali umeshapata na unagundua unaweza kuwa unao au hauna. Sio tatizo kubwa.
    Unashanga si ndiyo eeh...!
    Ni hivi...
    Haijalishi uko wapi na unafanya nini kama ni sehemu ambayo watu wapo basi unahitaji ukipata kati ya aina tano hizi za Marafiki basi usiwapoteze kabisa maana ni zaidi ya Tanzanite...
    ...pale machimbo ya Mererelani Arusha.
    Unataka kuwajua aina hizi za marafiki.
    Hata usiogope...
    Ndiyo maana,
    Nimekuandalia episode ya moto sana katika “Maisha Ni Kuthubutu Podcast” ujifunze zaidi kwa urahisi na kuelewa kwa kina.
    Baada ya Kusikiliza pengine utajutia kwanini sikuiweka episode hii mwaka mmoja au miaka iliyopita! Muda sahihi ni sasa ndio sababu ya kusoma hapa.
    Una sekunde 4 tu za kubofya link hapa chini Kusikiliza episode hii ili ujue aina 5 za Marafiki ambao ukiwa nao usiwapotezee.
    16 min
  • Sababu Kuu 04 Za Kwanini Unachepuka...?
    Hivi unajua kwamba asilimia 20% watu wanachepuka kwenye mahusiano yao, asilimia 30% wapo katika mahusiano ambayo wameyachoka tayari...
    Asilimia 20% wapo kwenye mahusiano na mume au mke wa mtu, asilimia 15% wapo single lakini wanachepuka na Ex wako. Asilimia 5% wapo single na asilimia 10% tu ndiyo wanafurahia mahusiano yao.
    Tatizo la kuchepuka ni tatizo kubwa sana ambalo si wanawake au wanaume kiwango cha kuchepuka kinaongezeka siku hadi siku.
    Swali la kujiuliza...
    Kwanini unachepuka?
    Kuna sababu nyingi ambazo zinafanya watu kuchepuka ukiachana na suala la fedha, kuna sababu zifuatazo;
    1. Kukosa tendo la ndoa (Sex) kwa muda mrefu
    Labda mwanaume ana changamoto ya nguvu za kiume au mwanamke ana tatizo la nguvu za kike, kukosa tendo kwa muda mrefu ni sababu moja wapo mtu kuchepuka si ndiyo.
    2. Ubize,
    Huwezi kuwa bize kiasi kwamba unashindwa kukaa karibu na mtu anayempenda, tatizo la kuwa bize inafanya mtu kuchepuka ili apate tulizo la moyo kwa kujaliwa, kuona anapendwa, kupewa thamani n.k
    3. Kati ya mmoja wapo kuchepuka,
    Mahusiano mengi watu wanachepuka kama Tukio la kulipa kisasi baada ya mpenzi mmoja kibaini anasalitiwa.
    4. Kokosa kujaliwa,
    Hisia zina nguvu sana mtu anapokosa kwa muda mrefu kujaliwa anaona akichepuka basi atakuwa atapata kujaliwa n.k.
    Ni baadhi ya sababu ambazo zinafanya mtu kuchepuka si ndiyo eeh!
    Basi Kama hupendi tabia ya kuchepuka una njia moja pekee ya wewe kutoka kwenye kifungo hiki ni Kusikiliza episode ya 21 ya “Maisha Ni Kuthubutu Podcast”.
    Bofya link hapa chini ujifunze kwa kina zaidi maana dakika 14 kutoka sasa utaenda kujua kwanini unachepuka na nini ufanye ili uache kuchepuka.
    15 min
  • Faida Za Kuandika ‘TO DO LIST’ Ya Kutimiza Malengo Yako.
    Umekuwa unashindwa kutimiza malengo yako na kuishia kupoteza hamasa ya kuendelea kupambana kwa kuona haiwezekani?
    Una malengo makubwa sana ambayo unaona haiwezekani kuyatimiza?
    Sio kosa lako.
    Kwa sababu siyo wewe pekee yako ambaye unashindwa kutimiza malengo yako.
    Lakini...
    Tatizo kubwa kwa kushindwa kutimiza malengo yako inafanya watu wengi inawezekana Hata wewe unaweka visingizio kuwa siyo mwaka wako labda mwakani ndiyo wako, unalalamika kila wakati kutafuta huruma ya watu wengine. Ukweli haisaidii zaidi unakaribisha UMASKINI na MAJUTO.
    Umeamua kabisa kughairisha na kusema mwakani ndiyo utapambana, kwani haujui kesho siyo yako na yako sio kesho?
    Habari njema ni kwamba...
    Hata kama umepoteza hamasa na nguvu ya kuendelea, basi TO DO LIST itakupa nguvu ya kuendelea kupambania malengo yako makubwa kwa kutumia nguvu kidogo.
    Ni hivi....
    Unaweza kumla tembo mzima kwa muda mchache kama utamkata vipande vidogo vidogo Ina maana kuvunja malengo yako mkubwa kuwa malengo madogo madogo.
    Sasa TO DO LIST itakusaidia katika siku yako kuwa na vipaumbele Muhimu juu ya kazi au majukumu ambayo ukiyatimiza unasogea hatua kadhaa mbele kutimiza malengo yako.
    To do list ni orodha ya kazi ambazo unategemea utafanya katika siku husika. Na inapangwa kwa kuzingatia umuhimu wa kazi na matokeo ambayo utapata kwa kukamilisha kazi.
    Faida ya kuwa na To do list inakusaidia kutopoteza muda wako kwenye mambo yanayokuweka mbali na malengo yako.
    By the way, kujua kuandika to do list imeelezwa katika Podcast ya maisha ni kuthubutu ambayo utajua Faida zake kwa kina na namna ya kuandika kwa Njia rahisi kabisa, Cha kufanya Bofya link hapa chini kusikiliza.
    13 min
  • Jinsi Akili Yako Inavyofanya Kazi Na Namna Inaweza Kuboresha Maisha Yako.
    Akili yako inawajibika kupokea, kutunza na kuchakata TAARIFA ambazo zinatoka sehemu mbalimbali za mwili.
    Akili haipimwi kwa alama za darasani.
    Akili haipimwi kwa cheo ambacho mtu anapata.
    Akili haipimwi kwa umri ambao unao.
    Akili haipimwi kwa kukubalika na watu.
    Kwa bahati mbaya....
    Hakuna sehemu ambayo wanaeleza jinsi gani akili inafanya kazi zaidi ya kukueleza kuwa na fikra au mawazo chanya si ndiyo?
    Kumbe akili yako ni zaidi ya wewe unavyofikiria kuwa una akili, hebu jiulize ni kitu gani kinaonyesha una akili?
    Majibu yako utajua sahihi au siyo kwa kuendelea kusoma.
    Lakini akili yenyewe inafanyia kazi TAARIFA ambazo zinakuwa zipo katika mfumo wako akili, kabla ya kuniuliza ni kwa namna gani?
    Ni kwamba kuna tofauti Kati ya akili (mind) na mfumo wa akili (Mindset).
    Kabla sijelezea kwa kina tofauti...
    Hebu fahamu aina mbili za akili ambazo zinaweza kuboresha maisha yako kama utajua namna ya kuzitumia;
    1. Conscious mind.
    2. Subconscious mind.
    Hizi ni akili ambazo zinafanya Uwe wewe wa leo na unaweza kutumia akili yako kuwa mtu ambaye unamtaka kwa kuelewa kitaalamu akili hizi zinafanyaje kazi.
    Upo tayari kujua namna gani akili yako inaweza kuboresha maisha yako na kuelewa namna Inavyofanya kazi.
    Okeeey!
    Ni rahisi sana kujua ni wewe Kusikiliza episode ya dakika 17 itayoenda kufanya maisha yako yote kuwa mtu ambaye unamtaka.
    Bofya link hapa chini kusikiliza madini haya sasahivi .
    18 min
  • Sababu Nne (04) Za Kwanini Unashindwa Kutimiza Malengo Yako.
    Unaweza kutimiza malengo yako, kama utajua mbinu sahihi ambazo ni chachu ya kutimiza malengo yako.
    Lakini...
    Kuna sababu ambazo zinafanya watu wengi washindwe kutimiza malengo yako, inawezekana hata wewe mwaka 2022 ulishindwa kutimiza malengo yako kwa sababu fulani fulani si ndiyo?
    Kutimiza malengo siyo ajali bali ni mchakato mtalaamu.
    Kati ya sababu hizi inaweza kuwa chachu ya kushindwa kutimiza malengo yako;
    1. Kutojua umuhimu wa kuwa na malengo,
    Unaishi kwa mazoea kutojua umuhimu wa malengo, kwa sababu Hakuna shule au chuo inafundisha umuhimu wa kuishi kwa malengo katika maisha yako, na kuishia kuwa na ndoto na matamanio tu.
    2. Kutojua umuhimu wa kupanga malengo yako,
    Kwa sababu wengi hudhani wana malengo SMART kumbe wana ndoto na matamanio tu, katika Podcast ya maisha ni Kuthubutu nimeleza namna ya kupanga malengo SMART kwa kina, chukua muda sikiliza.
    Jiulize maswali yafuatayo;
    Je, malengo yako umeandika?
    Je, umeweka mipango thabiti?
    Je, umeweka deadline kujua lini utatatimiza malengo yako?
    Je, umevunja malengo makubwa kwenda malengo madogo madogo?
    Je, unajua hatua gani uchukue ili utimize malengo yako?
    Ni baadhi ya maswali ambayo ni Muhimu kujiuliza wakati unapanga malengo yako?
    3. Hofu ya kufeli,
    Kuna Hofu ya kuanza na Kuthubutu kupambana kutimiza malengo yako, kuna Hofu inafanya ushindwe kupiga hatua, Je unajua hofu inayokusumbua?
    Kwahiyo...
    Ni baadhi ya sababu ambazo zinafanya ushindwe kutimiza malengo yako, baada ya kujua sababu hizi umekuwa chachu ya kutimiza malengo kwa asilimia 94% na zaidi
    Kwa sababu nataka utimize malengo yako kutoka sasa si Upo tayari si ndiyo eeh! Basi ni simpoooo...
    Bofya link hapa chini Kusikiliza episode ya 18 hapa chini una dakika 18 za kutimiza malengo yako kuanzia sasa na kuendelea...
    19 min
  • Tabia Tano (05) Za Kuepuka Ili Utimize Malengo Yako.
    Tabia Ina nafasi ya moja kwa moja ya wewe kutimiza au kutotimiza malengo yako, kwa bahati mbaya watu wengi wanachukulia poa sana suala la tabia.
    Ukitazama elimu kuhusu tabia gani zinaleta mafanikio na kutimiza malengo yako kwa kishindo haitolewi kwa ukubwa zaidi katika mazingira ambayo tupo.
    Unauliza “Innocent” ni kwa namna gani?
    Swali zuri Mtaalamu.
    Ni hivi....
    Kuna tabia ambazo zilifanya utimize malengo yako ya mwaka 2022?
    Kuna tabia ambazo zilifanya ushindwe kutimiza malengo yako ya mwaka 2022?
    Vizuri, kwa kupata majibu na umeanza kuona tabia Ina nafasi kubwa ya kutimiza au kutotimiza malengo yako.
    Kwa mifano;
    Mfano wa kwanza. Je mtu ataweza kupungua uzito akiwa na tabia ya kula ovyo vyakula vya mafuta, Sukari na ana tabia ya kutofanya mazoezi?
    Jibu ni hapana! Kumbe tabia hizi ni kikwazo.
    Mfano wa pili: Mtu anataka kuwa na kiasi cha millioni moja mwisho wa mwaka na akawa kila mwisho Mwa mwezi kwenye akaunti anaweka laki moja kama akiba, Atafanikiwa kufika lengo Lake mwezi disemba.
    Kumbe tabia ya kuweka akiba ni chachu ya kufikia lengo la kifedha si ndiyo mtaalamu?.
    Lakini...
    Leo utajua tabia gani za kuepuka ili utimize malengo yako, ukweli kuna tabia fulani fulani ambazo ukiziepuka ni suala la muda wewe kutimiza malengo yako, kama unajitihada.
    Unataka kujua tabia gani uepuke si ndiyo?
    Sekunde chache kutoka sasa utaenda kujua tabia hizi ndani ya podcast ya Maisha ni kuthubutu...
    ....maana huku umepewa kila kitu katika episode hii ambayo Ina dakika 19 tu za kufanya mwaka huu kuwa wako wa kutimiza malengo yako.
    Cha kufanya ni rahisi.
    Bofya link hapa chini sasahivi usikilize episode hii na utajutia kwanini hukusikiliza miezi sita iliyopita, hujachelewa Bofya hapa chini Mtaalamu upate madini.
    20 min
  • Jinsi Kanuni Ya 3K’s Inavyojenga Hatima Ya Maisha Yako.
    Watu ni hodari wa kupanga mipango kikubwa si ndiyo?
    Watu ni hodari sana wa kupanga malengo makubwa si ndiyo?
    Una Kumbuka hata siku ya mwaka mpya ulipanga malengo makubwa na kusema huu ni mwaka wako si ndiyo?
    Lakini...
    Watu wengi licha ya kujua kupanga, wanashindwa sehemu mbili ambazo ni;
    1. Kuamua/kuthubutu.
    2. Kutenda.
    Hebu fikiria ukiamua kupambania mipango na malengo yako utakuwa wapi?
    Haitoshi si ndiyo...
    Ni lazima utende kwa maana kuchukua hatua (To take take actions) baada ya kuamua kupambania malengo yako si ndiyo?
    Kwahiyo....
    Leo utaenda kujua kanuni ya 3K’s ambayo itaenda kubadili hatima yako na kuwa mtu mwingine tena...
    Kuanzia uthubutu wako utaongezeka kwa kiwango cha juu sana.
    Kiwango cha kutenda (taking actions) utaongezeka mara kumi 10X zaidi sasa.
    Kwa sababu kanuni hii inafundishwa kwa hela nyingi kwa maana ya tsh 50,000.
    Ila...
    Leo utaipata bure kwenye Podcast ya Maisha ni kuthubutu” ambayo ndani ya dakika 13 tu utajifunza elimu hii ambayo itaenda kuwa chachu ya kujenga hatima yako.
    Ni wewe tu kuifanyia kazi baada ya muda utanipa ushuhuda wako.
    Cha kufanya ni rahisi kabisa...
    Ni kubofya link hapa chini sasahivi kusikiliza episode hii na upate madini ya nguvu. Usichelewe chukua hatua sasa.
    14 min
  • Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Ya Mwaka 2023.
    Kabla ya kusema mwaka 2023 ni mwaka wa wewe kupiga hatua na kufanikiwa kwa kiwango cha juu kwa kutimiza malengo yako.
    Jiulize mpaka sasa, umeshapanga malengo yako ya mwaka 2023?
    Au.
    Unataka kupiga hatua lakini Hakuna hata malengo ambayo umeandika kwenye diary yako, nikuambie haupo “Serious” kabisa.
    Hebu kuwa Serious kidogo basi...
    Sababu unakuwa bado hauna malengo, badala yake unakuwa na matamanio na ndoto za kutaka kitu fulani pasipo kujua namna ya kupata.
    Ni hivi...
    Kupanga malengo yako kiusahihi na kuyaandika malengo yako unaongeza nafasi ya kufanikiwa kwa asilimia 42% kuliko ambaye hajaandika kabisa malengo yake.
    Kwahiyo...
    Kama Unataka mwaka 2023 Uwe mwaka wa kupiga hatua, kuna namna sahihi ya wewe kupanga malengo yako ambayo inafanya kazi kwa watu wote duniani.
    Sababu utakuwa na mwelekeo sahihi wa nini ufanye Ili utimize malengo yako.
    Utaenda kujua hatua ya “Systematic Approach” ambavyo itakusaidia kuvunja lengo kubwa kuwa malengo madogo madogo, ili uwe na ufanisi mkubwa wa kutimiza malengo yako.
    Utajua ni kwa namna gani “Your thoughts” kwa maana mtazamo wako ni Muhimu katika kutimiza malengo yako.
    Utajua namna ya kupanga mipango inayoeleweka na inapimika “Clear plans” katika kutimiza malengo yako.
    Utajua namna gani ya kuandaa mpango kazi wa kuchukua hatua kutimiza malengo yako “Actions plan”.
    Utajua yote kwa Kusikiliza episode ya 15 ya “HATUA SABA (07) ZA KUZINGATIA WAKATI UNAPANGA MALENGO YA MWAKA 2023”.
    Cha kufanya ni kitu kimoja rahisi...
    Ni kubofya link hapa chini sasahivi Kusikiliza episode hii ya moto ambayo ina dakika 18 za kufanya mwaka 2023 uwe mwaka wa kutimiza malengo yako.
    22 min

About Maisha Ni Kuthubutu Podcast

From the publisher's feed

Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha.