Maisha Ni Kuthubutu Podcast

Maisha Ni Kuthubutu Podcast

By Innocent NgaohEducationSelf-Improvement
Download on the App Store

Maisha Ni Kuthubutu Podcast episodes

  • Uchambuzi Wa Kitabu Cha MONEY FORMULA (Kanuni Za Fedha)...!
    Elimu ya fedha isiyofundishwa shuleni wala vyuo vikuu imepelekea kushindwa kupiga hatua kwenye eneo la fedha.
    Kitabu cha MONEY FORMULA kinakupa mwongozo sahihi ni kwa namna gani unaweza kufanikiwa kifedha kupitia sheria, kanuni na mitazamo sahihi kuhusu fedha.
    Hakikisha unafanyia kazi ambayo unajifunza.
    30 min
  • Uchambuzi Wa Kitabu Cha "BIRD BY BIRD"
    Ni kitabu mahususi kimeandikwa na Anne Lemmot ambacho utajifunza mambo mengi kuhusu uandishi wa vitabu na kuishi maisha yenye uhuru ndani yake.
    Hakikisha unaandika pembeni mambo ambayo utajifunza kupitia uchambuzi wa kitabu hiki kizuri cha BIRD BY BIRD yaani NDEGE KWA NDEGE.
    Katika uchambuzi wa kitabu hiki utajifunza sura tano ambazo mwandishi ametushirikisha kuhusu uandishi wa vitabu na ndani ya sehemu hizo zimegwanyikwa part ndogo ndogo.
    Ni kitabu kizuri kama unataka kuwa mwandishi mzuri wa Riwaya, Hadithi, Simulizi, Makala Na Vitabu Aina Yoyote basi uchambuzi ni mahususi kwako.
    Kitabu cha BIRD BY BIRD ni kitabu kizuri basi unahitaji sana kusoma kitabu hiki.
    Kurahisha nimekuandalia mambo yote muhimu kuhusu kitabu kwa lugha hadhimu ya Kiswahili.
    Hakikisha una SUBSCRIBE podcast hii
    32 min
  • Ufanye Nini Unapitia Hali Ya Kutoeleweka Katika Mapambano Au Utafutaji Wako?...
    Usijisikie vibaya kuona watu wa karibu au wa mbali hawaelewi wala hawapo tayari kukuelewa kuhusu mapambano yako.
    Inaumiza kuona watu ambao unawapenda na kuamini inaweza kuwa,
    ๐Ÿ“Œ Wazazi wako,
    Ulitegemea ndiyo wangekuwa watu wa kwanza kukuelewa na kuamini unachofanya na imekuwa tofauti wanakukosoa na kukalaumu kwanini unafanya hicho.
    ๐Ÿ“Œ Marafiki zako,
    Marafiki ambao umeshindana nao muda mwingi wanakuwa hawaamini unachofanya na hawaelewi mapambano yako na kuona unapoteza muda au pengine unapoteza muda au hutopata matokeo.
    ๐Ÿ“Œ Viongozi au boss wako,
    Inawezekana ni watu ambao unataka waelewe juhudi na kujitoa tofauti ila inakuwa tofauti wanakuwa hawaelewi na zaidi wanaona hujielewi inaumiza sana.
    ๐Ÿ“Œ Ndugu zako,
    Ndugu wanakuwa watu wa kwanza kukubeza na kuona kama umerukwa na akili kwa kuwa unafanya tofauti na matarajio au matazamio yao, pasipo kujua una ndoto zako na siyo ndoto zao.
    ๐Ÿ“Œ Mpenzi wako,
    Ulitegemea mpenzi wako angekuwa mtu wa kwanza kukusapoti, kukuhamasisha, kukushika mkono na kuelewa mapambano yako ila imekuwa tofauti amekuwa mbali na wewe, na kuishia kupata mashaka anakupenda kweli au yupo kwako ila mapenzi hayapo kwako?
    Pasipo kujali ni watu ambao hawaelewi unachofanya isiwe sababu ya kukata tamaa na kuona labda unachofanya siyo sahihi.
    Kwa sababu...
    Siyo lazima wakuelewe ila ni Muhimu kujielewa na kuelewa unachofanya ndiyo jambo la muhimu zaidi.
    Kuwa na mtazamo chanya kuwa unachofanya ni sahihi katika eneo sahihi ni suala la muda utapata matokeo.
    Wasipokuwa tayari kuelewa mapambano yako, basi wataelewa mafanikio yako, Kwahiyo endelea kupambana mpaka kieleweke.
    Inaumiza sana kuona hawaelewi, Naelewa maana sisi ni mashuhuda kwenye mapambano tunayofanya wanasubiri kuona mwisho wetu utakuwa upi.
    Ila MUNGU alivyo wa ajabu anatuketisha kwenye meza na wakuu.
    Amini unachofanya na JUHUDI siku zote haziganganyi na siyo lazima wakuelewe kwenye kila kitu ndiyo Maisha yalivyo rafiki yangu.
    Inawezekana unataka wakuelewe kwenye,
    1. Kipaji chako,
    2. Mawazo yako,
    3. Biashara yako,
    4. Ubunifu wako,
    5. Huduma yako, n.k.
    Endelea kupambana hata kama hawakuelewi maana kuna wengine hawataki kukuelewa si kwamba unafanya kitu kibaya laasha!
    15 min
  • Kabla Ya Kuingia Mwaka 2024 Hakikisha Unafanya Haya..!
    Umepanga kufanya maajabu mwaka 2024 na umejipanga vizuri kuanzia kupanga malengo yako, ndoto na maono yako. Lakini kuna vitu unapaswa kuzingatia kufanya leo hii kabla ya kuingia mwaka 2024. Utajifunza mambo 05 ambayo yatakusaidia kujua nini ufanye kabla ya kuingia mwaka 2024.
    17 min
  • ISHI KAMA KINYONGA....!
    Unajiuliza uishi kama kinyonga ni kwa namna gani si ndiyo? Ni kwamba unahitaji kuwa makini na kuishi kwa tahadhari kama kinyonga na watu wanakuzunguka hasa watu wa karibu yako. Hata wahenga wanasema โ€œAdui hatoki mbaliโ€ Sikiliza dakika 9 zenye kukupa mwanga na mabadiliko kwenye Maisha yako. Ushindwe wewe tu rafiki.
    10 min

About Maisha Ni Kuthubutu Podcast

From the publisher's feed

Podcast mahususi kujifunza mambo ya maendeleo binafsi (Personal development/Self-improvement), maisha, mahusiano, saikolojia na elimu ya fedha.