Men The Podcast

Men The Podcast

Download on the App Store

Men The Podcast episodes

  • Ep 40 - My Time in Prison
    Kutana na Tito Magoti, mwanasheria kijana kutoka Tanzania. Mwaka 2019, alijikuta gerezani ambapo alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Sasa Tito ametoka, anaendelea na maisha yake.
    Unahitaji nini ili uweze ku “survive” maisha ya gerezani? Watu wako wanaokuzunguka inabidi wafanye nini ili waweze endelea kukutia moyo? Nini kilichompa Tito nguvu na moyo wa kuishi gerezani na kumfanya asikate tamaa ya maisha? Baada ya kutoka gerezani, jamii imempokeaje Tito? Yupo tayari kuishi maisha ya mtu anayeangaliwa sana na jamii kila anapokwenda? Gerezani kumembadilisha vipi Tito? Na zaidi ya yote, vipi kuhusu afya ya akili magerezani?
    Maswali ni mengi sana kutoka kwa Michael Baruti pamoja na Mwanasaikolojia Nadia Ahmed, karibu usikilize maongezi haya.
    1 hr 9 min
  • Ep 39 - Men do communicate, differently

    Wanaume hawajui namna ya bora ya kuwasiliana, kuanzisha mazungumzo ya muhimu na inawezekana hawajui kabisa kuongelea wanayoyapitia, wanayoyafikiria au kuelezea hisia zao wakiwa kwenye mahusiano, hii ni dhana iliyojengeka kwa watu wengi sana, je ina ukweli wowote?

    Baadhi ya wanaume wanapingana na hili, na wanasema si kweli. Wanaume wanaweza sana kuwasiliana, sema tu wanawasiliana kwa namna ambayo ni tofauti na inahitaji muda kuielewa.

    Michael na Nadia wanazungumza kwa kirefu sana na Gillsant pamoja na Leslie juu ya mawasiliano, matarajio na changamoto za kutokuwa na mawasiliano mazuri kwenye mahusiano kwa upande wa mwanaume na namna gani mawasiliano yanaweza kujenga au kubomoa kabisa mahusiano hayo.

    1 hr 46 min
  • Ep 38 - Ukweli kuhusu nguvu za kiume

    Tatizo la nguvu za kiume ni tatizo gani? Linaathiri wanaume wangapi duniani? Chanzo cha hili tatizo ni nini? Matumizi ya dawa za asili kama “Vumbi la Congo” na “Al Kasusi” ni kweli yanasaidia kutatua tatizo hili? Ni tatizo linalotibika? Kuna madaktari wanaoweza kusaidia kwenye hili tatizo? Linahusiana vipi na afya ya akili? Mbona mara nyingine hili tatizo kama linapotea na mara nyingine kama linarudi? Kuna suluhisho la kudumu?

    Haya ni baadhi ya maswali ambayo wanaume wengi sana hujiuliza kuhusiana na “Nguvu za Kiume”. Katika nia ya kujenga na kuboresha afya ya akili kwa wanaume, episode hii imeamua kuzungumzia hili tatizo kwa undani tukiwa na matumaini kwamba kwa yeyote atakayesikiliza basi ataweza kupata taarifa za kina na taarifa sahihi.

    Michael pamoja na Nadia wamefanya mazungumzo ya kina na “Urologist” kutoka Tanzania, Dr Boio Nyamwihura ili kupata ukweli na taarifa zaidi kutusu mwanaume na “nguvu za kiume”

    1 hr 12 min
  • Ep 37 - Seemingly perfect? Think again (Part 2)
    If you were asked the following questions; do you think you have mastered the art/science of life and communication? What does conflict resolution in your relationship(s) look like? Do you think it is possible to love the things that you’ve grown to hate? And lastly but most importantly, what's the importance of self-acceptance and self-awareness in our life journey? - Would you know the answers at the tip of your finger?
    Welcome, we are thrilled to have you back with us in this second part of our conversation with Princely Glorious. In this episode, Princely opens up on how he dealt with anxiety, what he has learnt to be the best way to communicate his thoughts and solve conflicts with his partner, how to disagree respectfully but also how stepping out of your normal routine and halting the things that matter to you could be a sign of anxiety. Join us as we unravel, learn and speak on this part of Mental health.
    57 min
  • Ep 36 - Seemingly perfect? Think again (Part 1)
    Look, Princely anaendesha kampuni nzuri inayofanya vizuri kibiashara, kampuni yake ilishinda shindano na wakapata hela nzuri tu ya kumwezesha yeye kuendelea kutimiza ndoto zake. Anaishi kwenye eneo zuri, na ni mtu poa sana. Hawezi kuwa na tatizo, na afya yake ya akili haiwezi kuwa challenged, right? WRONG
    Ukweli ni kwamba, si mara zote tuonekanavyo nje ndiyo tulivyo kwa ndani. Unaweza onekana kwamba una kila kitu nie, ila bado afya ya akili isiwe katika mahali sahihi. Inakuathiri vipi? Unatambuaje hilo? Unapambana halo kwa namna gani? Haya ni maongezi na Princely Glorious, mwanaume aliyeamua ku-share na sisi experience yake kwenye hili
    1 hr 2 min
  • Ep 35 - Three Months Paternity Leave

    Miezi mitatu ya likizo ya uzazi kwa mwanaume. Inaonekana kama kitu cha ajabu sana hata kukizungumzia, uongo au kweli?

    Can you imagine a man, a Tanzanian man to be precise taking three months paternity leave? Well, kama hauamini basi fahamu kuwa yupo mtu aliyefanya hivyo, na muda huu ulibadilisha kabisa maisha yake na mtazamo wake kwa ujumla juu ya uzazi na malezi kwa ujumla.

    Lakini pia tunazungumzia kwanini wanaume walio wengi hupata changamoto kubwa pale wanapopata watoto wachanga na namna gani jamii inayotuzunguka (ndugu na marafiki) inaweza kuwa na nafasi kubwa sana ya kukufanya utumie muda mwingi zaidi na familia yako pale unapobahatika kupata mtoto mchanga ili kusaidia kujenga familia bora zaidi.

    1 hr 20 min
  • Ep 33 - Blended Family, Fatherhood & Therapy

    Moja kati ya mambo ambayo yapo kwenye jamii zetu ila hayazungumziwi sana ni namna ya kuweza kuwa baba bora na mume bora pale ambapo unaishi katika familia iliyochanganyika (Blended Family).

    Lakini ni namna gani unaweza kufikia hilo lengo pale ambapo kuna zaidi ya baba mmoja kwenye familia, zaidi ya mama mmoja, zaidi ya bibi na babu mmoja kwa kila upande na zaidi ya mtoto mmoja ambar yupo katikati ya haya yote?

    Michael na Nadia wameingia ndani na kulijadili hili kwa kina na ndugu Reuben Ndege anaefahamika zaidi kama Ncha Kalih

    1 hr 23 min
  • Ep 32 - Unpacking The Man Box

    “The man box” Hili ni box ambalo sio rasmi, na limetengenezwa na Jamii linalotumika kuchanganua tabia za mwanaume. Kwenye box hili kuna mazuri kuhusu wanaume, lakini pia kuna vitu ambavyo sio sahihi kuendelea kuvishikilia kwa mwanaume anaetaka kubadilika na anaetaka kuwa bora.

    Lakini, nani alianzisha “box” hili? Mambo gani mazuri yanayopatikana katika hili box? Yepi ambayo si mazuri na hayafai? Na pia, namna gani wanaume tunaweza kuanza kuchambua na kutoa yasiyofaa kutoka kwenye hili box?

    Ungana na Michael, Nadia pamoja na Sadick Ali ambapo kwa wiki hii wameamua kulifungua hili box ili Jamii yote ipate kuona yaliyo ndani yake.

    59 min
  • Ep 31 - How Do You Move On From A Big Loss?

    KIla kitu kilikua kinaenda vizuri sana kwa Gabriel, wakati akiwa anasoma chuo kikuu alibahatika kupata mwenza wa maisha. Wakajaliwa mtoto mzuri wa kiume, na baada tu ya kumaliza chuo wote wawili wakaamua kufunga pingu za maisha. Familia nzuri, na changa hii ni ndoto ya watu wengi, si ndiyo?

    Lakini, wakati wa taratibu za kujifungua mtoto wa pili, mke wa Gabriel anafariki, na mtoto anapona.

    Katika umri mdogo wa miaka 30, Gabriel anapoteza mwenzi wake wa maisha, na anaachiwa watoto wawili ambao inabidi awape malezi. Ni vipi anafanikiwa kuendelea na maisha yake?

    1 hr 14 min
  • Ep 30 - Lessons From My Father
    Vuta picha, wewe ni kijana mdogo wa kiume, una miaka 7, unaishi na baba na mama na wadogo zako. Baba ni mwanasheria anayechipukia kwa kasi sana katika Serikali ya nchi changa ya Tanzania, mnaishi kwenye nyumba zuri ya hadhi ya juu na kila kitu kipo sawa.
    Then linatokea janga kubwa sana katika familia, unapoteza wadogo zako wote, mama anapelekwa jela na wewe unalala hospitali kwa miezi kadhaa ukiwa haujitambui. Pindi tu unapopata fahamu, baba anakuchukua unaenda kuishi nae nje ya nchi mkiwa mpo wawili tu, wewe na yeye.
    Hii ni story ya Taji Liundi. Anazungumzia namna gani milima na mabonde aliyovuka na baba yake. Na namna gani experience hii imechangia kumfanya awe namna alivyo sasa hivi.
    1 hr 21 min

About Men The Podcast

From the publisher's feed

One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life.