Tunazungumzia ugonjwa wa Ebola ambao unaendelea kuripotiwa nchini Uganda ukiwa ni mlipuko wa tano. Watu 24 wamepoteza maisha huku ugonjwa huu ukiendelea kusambaa. Aina hii ya Ebola Sudan japo haijaripotiwa kusababisha vifo vingi kwa haraka kama vile Ebola Zaire iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,bado haina chanjo.
Mataifa majirani kama vile Rwanda ,Tanzania na Kenya kutokana na hali hii zimeanza kuweka mikakati ya kukabiliana na hali ya dharura