Msasa Media

Msasa Media

By Msasa MediaNewsDaily News
Download on the App Store

Msasa Media episodes

  • TABIA ZA WATU WENYE USALITI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI.
    Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja.wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa.
    Siku zote anaekusaliti huwa anajiona mjanja sana, kwamba yeye anasaliti mwenza wake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi nb wao wasithubutu kuwasaliti.
    Kwanini hawataki wenza wao wasaliti? eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa.
    kusaliti asaliti yeye akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa
    Anajisikia fedheha kwamba Mpenzi wake amemuonaje? amemchukuliaje?hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hicho inamtazamaje?.
    Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake.
    Zifuatazo ni dalili za usaliti.
    1. KUTOPENDA KUFATILIWA KIUNDANI.
    Mara nyingi anaekusaliti hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, anahofu anaweza kuchanganya madawa, hapendi mazungumzo mafupi ya moja kwa moja.
    Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayoyataka yeye.
    Ukimuuliza Kuhusu mipango yenu, ukimuuliza Kuhusu mustakabali wa mahusiano yenu hawezi kukujibu moja kwa moja baada huku ondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza.
    2. HAPENDI UJUE RATIBA ZAKE.
    Mara nyingi mtu ambaye ana mambo yake hapendi ujue ratiba zake, anataka usimzoee ,iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyotaka, ikitokea unaijua ratiba yake atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati.
    Leo atakwambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona, kesho atakwambia kuna kikao cha wafanyakazi wenzake, siku nyingine atakwambia gari imepata pancha analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari.
    3. SIMU YAKE NI KITUO CHA POLISI.
    Anayesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela, simu inakaa mfuko kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo mpo nyumbani kwenye kikao cha mazungumzo ya kifamilia yeye simu yake ipo mfukoni.
    Imetolewa mlio hataki usikie ikiita, au ujumbe ukiingia ,au picha na mambo mengine ya kimapenzi.
    Anayejiamini na yupo kwenye uhusiano imara hana sababu ya kuficha ficha simu yake au kuweka paswedi kila mahali simu yake anaiweka hadharani.
    Mwingine anakusetia simu yake ukimpigia kila wakati inaonekana inatumika wakati huo anakusaliti.
    4. ANACHATI SANA.
    Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao, yaani anawazoesha michepuko yake wote kusaliti hapendi kupokea simu zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuchati na wapenzi wengine bila wewe kujua na kufuta meseji zote ili hata ukishika simu kwa bahati mbaya usizione na usigundue kitu.
    Mwisho hakutambulishi kwa watu wake wa karibu, ukiona mpenzi wako hajawahi kukutambulisha kwa rafiki zake, ndugu zake na watu wengine wa karibu ujue hapo hamna muelekeo wa mapenzi yenu tafuta njia mapema ya kujiundoa kabla ya kupotezewa muda wako.
    Kwa haya machache natumaini utakuwa umeshafahamu Mpenzi wako uliyenae kwa sasa ana malengo gani? na je anakusaliti ama ni mwaminifu ili uweze kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika.
    4 min
  • FAIDA 8 ZA KUWEKA AKIBA UNAZOPASWA KUZIFAHAMU.
    1. Uhuru wa kifedha.
    Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na fedha, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani.
    Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye suala la uhuru wa kifedha,ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi.
    Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha.
    2. Matumizi mazuri ya pesa.
    Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa kuweka akiba sio kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi na mipango stahiki pekee.
    Hivyo kuweka akiba kutakufaidisha kwa kukuwezesha kutumia pesa vyema.ikiwa unapata elfu 10 kwa siku,itakubidi uitumie vizuri ili uweze kutenga pesa ya akiba.
    Kama huweki akiba huna haja ya kutumia pesa vyema kwani hakuna sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa.
    3. Kujiandaa kwa dharura
    Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile magonjwa, misiba majanga n.k
    4. Kuweza kufanya manunuzi au miradi ya gharama kubwa
    Kuna manunuzi au miradi inahitaji pesa nyingi ili kuitekeleza. Maswala kama vile ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja kununua gari n.k, ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi.
    Hivyo,kwa kuwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi kuliko ungeyafanya bila akiba.
    5. Kuweza kumudu wanaokutegemea
    Ikiwa kuna watu wanaokutegemea kama vile wazazi, ndugu au watoto ni vyema kuweka akiba ili uwe na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatwapo na uhitaji.
    Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na huko ili kutafuta pesa ya kukidhi mahitaji ya wategemezi wako kama vile chakula, matibabu au hata ada za shule.
    6. Utulivu wa akili
    Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili, Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuwaje? au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni itakuwaje?n.k
    Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwa unajua hata ukikosa pesa akiba yako itakusaidia.
    7. Hukuwezesha kuandaa kesho vyema
    Maandalizi ya kesho yanafanywa leo.kuweka akiba maana yake unajiandaa na mahitaji ya kifedha ya baadaye yaani kesho.mtu asiye kuwa na akiba mara nyingi hafikirii Kuhusu kesho wala hamna malengo kwa ajili ya baadaye yake.
    Ili kujenga baadae au kesho njema,ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba.
    8. Hukuwezesha kuwahi fursa
    Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile" ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu",au "ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma" au "ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye huu mradi".n.k
    Hili kinadhihirisha watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya pesa,unapokuwa na akiba ya pesa ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.
    Hitimisho
    Fedha ni jambo linalohitaji nidhamu na busara ya hali ya juu, vivyo hivyo kuweka akiba ni swala linalohitaji kufanya maamuzi sahihi ili uweze kulitekeleza.
    4 min
  • MWINYI ZAHERA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI GWAMBINA FC.
    Mwinyi zahera ametambulishwa rasmi kuwa kocha Mkuu wa klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu wa 2019/20 na itashiriki ligi kuu Bara msimu wa 2020/21.
    Zahera aliwahi kuifundisha yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa.
    Kocha huyo amesaini dili la miaka 5 na inaelezwa kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga.
    Wanaotajwa kuibukia Gwambina ni pamoja na Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru.
    Vilevile Waziri wa michezo Tanzania, Dkt Harison Mwakyembe ametangaza uamuzi wa serikali kuendelea kuruhusu idadi ya wachezaji 10 wa kigeni huku idadi ya wachezaji wanaotakiwa kucheza itaratibiwa chini ya baraza la Michezo la Taifa BMT.
    Amesema bado wizara kwa kushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kikao kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia nchini.
    Amefafanua, "Angalau nchi zilizopo katika nafasi 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata kwa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tuu,ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka nje wawe na weledi na uwezo mkubwa.
    2 min
  • SOMALIA : WATU 10 WAUAWA KATIKA JARIBIO LA KUVUNJWA GEREZA.
    Mamlaka ya Somalia inasema watu 10 wamefariki wakati wa majibizano ya risasi nje ya gereza la Mogadishu.
    Msemaji wa wizara ya habari alisema mahabusu 6 ambao walikuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi Al-Shabab waliuliwa na askari wanne pia waliuawa.
    Chanzo cha majibizano ya risasi ni jaribio la mahabusu mmoja kutaka kutoroka.
    Kuna taarifa zinazosema mahabusu mmoja aliweza kupora bunduki kutoka kwa msimamizi wa gereza na baadae mahabusu na wafungwa wengine walivunja chumba cha kuhifadhia bunduki.
    Kikosi maalumu cha polisi kililelekwa kukabiliana na ghasia hizo ambazo zilikuwa zinalenga kuvunja gereza.
    Gereza hilo lina wafungwa ambao ni wanamgambo maarufu wa Al-Shabab ambao wanatumikia kifungo cha maisha au kunyongwa.
    2 min
  • TANZANIA : MR KUKU KIZIMBANI KWA KUFANYA BIASHARA HARAMU YA UPATU NA UHUJUMU UCHUMI.
    Mfanyabiashara,Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr kuku, amefikishwa mahakama ya kisutu, akikabiliwa na mashtaka 7 likiwemo la kufanya biashara haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Tsh. bilioni 17.
    Machibya amesomewa mashitaka yake tarehe 10.08.2020 na wakili mwandamizi wa Jamhuri, Simon Wankyo mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya.
    Mbali na shtaka la kusimamia biashara haramu ya upatu,Mr kuku anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pia ana mashtaka ya kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila leseni na kutakatisha fedha.
    Anatuhumiwa kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma aliwadanganya kuwa watafanya ujasiriamali wa ufugaji wa kuku na watapata faida ya asilimia 70 kwa waliowekeza kwa miezi 8 na asilimia 90 kwa waliowekeza kwa miezi 6, kiasi kinachoelezwa kuwa kikubwa kuliko mtaji uliokusanywa.
    Pia kati ya Aprili 26,2019,na Januari 26, 2020 jijini Dar anadaiwa kujihusisha na miamala ya Tsh. Bilioni 6.4 kutoka katika akaunti inayoitwa Mr. kuku pharmacy katika benki ya CRDB huku akijua fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya Upatu.
    Aidha anadaiwa kupokea fedha kiasi cha Tsh.Bilioni 17 ya maingizo ya umma bila kuwa na leseni. upande wa Mashtaka umesema upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 24,2020 huku mtuhumiwa akirudi rumande kutokana na makosa hayo kutokuwa na dhamana.
    2 min
  • RAIS GHANI WA AFGHANISTAN KUWAACHIA WAFUNGWA HATARI WA KUNDI LA TALIBAN.
    Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema atatoa amri ya kuachiwa huru kwa wafungwa 400 wa kundi la wanamgambo wa Taliban baada ya baraza la jadi la viongozi wa kikabila kuunga mkono hatua hiyo kama njia ya kufufua mazungumzo ya amani.
    Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kufunga mkutano wa baraza hilo linalojulikana kama 'loya jirga' amesema atatia saini amri hiyo kama ilivyotakiwa na kundi la Taliban na baada ya viongozi hao wa kikabila kufikia mwafaka.
    Uamuzi huo utaondoa kikwazo cha mwisho kilichotatiza kusonga mbele kwa mazungumzo ya kusaka amani kati ya serikali mjini Kabul na kundi la Taliban. Ghani alilazimika kuitisha kikao cha baraza hilo baada ya kushindwa kutoa idhini ya kuachiwa wafungwa hao 400 ambao wengi wanatuhumiwa kwa makosa makubwa ya jinai ikiwemo kupanga mashambulizi yaliyowaua maelfu ya raia Afghanistan na wageni.
    Vilevile Serikali ya Afghanistan na kundi la wanamgambo la Taliban wanakaribia kuafikiana kuhusu mazungumzo ya amani baada ya wawakilishi wa makabila kuidhinisha kuachwa huru wafungwa 400 waliokitovu cha mvutano kati ya pande mbili.
    Azimio hilo limefikia mwishoni mwa mkutano wa siku tatu unaofahamika kama 'loya jirga' unaowakutanisha viongozi wa kikabila na wawakilishi wa makundi mengine, mkutano ambao wakati mwingine huitishwa ili kutafuta majibu ya masuala tata.
    Mjumbe mmoja wa mkutano huo amesema kwa lengo la kuondoa vizingiti vya kuanza kwa mazungumzo ya amani na kukomesha umwagaji damu, baraza hilo limeridhia kuachiwa huru kwa wafungwa 400 kama kundi la Taliban lilivyotaka.
    Orodha ya wafungwa hao inajumuisha wale wanaotuhumiwa kwa makosa makubwa ya jinai ikiwemo kushiriki kwenye mashambulizi yaliyowaua maelfu ya raia wa Afghanistan na wageni.
    3 min
  • MALAWI : YATANGAZA VIZUIZI VIPYA VYA KUKABILIANA NA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA.
    Tarehe 09, Agosti, Malawi imetangaza kuyafunga makanisa yote na kumbi za starehe katika awamu mpya ya vizuizi vya kudhibiti ongezeko linalotia wasiwasi la Virusi vya Corona.
    Vizuizi vipya vilivyotangazwa Kupitia gazeti la serikali vinajumuisha pia amri ya kuvaa barakoa na marufuku kwa Mikusanyiko inayozidi watu 10 isipokuwa kwa shughuli za mazishi zitakazo ruhusu jumla ya watu 50.
    Mwanasheria Mkuu wa serikali Chikosa Silungwe, amesema kikosi maalumu cha maafisa wa jeshi kimeundwa kuhakikisha Masharti hayo mapya yanatekelezwa. Malawi haijatekeleza marufuku kamili ya shughuli za umma baada ya mahakama kuzuia mwezi Aprili nia ya serikali ya kuifunga nchi nzima kwasababu ilishindwa kutangaza msaada utakaotolewa kwa watu wasiojiweza.
    Tangu taifa hilo la Kusini mwa Afrika lililotangaza kisa cha kwanza cha Covid-19 mnamo Aprili 2, idadi ya maambukizi imepanda maradufu katika kipindi cha wiki nne zilizopita na kufikia visa 4,624 ikiwemo vifo 143.
    2 min
  • TETESI ZA SOKA KIMATAIFA.
    Washindi wa soka la FA Arsenal wana mlenga beki wa kati wa Brazil Diego Carlos huku Mikel Arteta akipanga marekebisho makubwa msimu ujao.(Telegraph - Subscription required).
    Arsenal itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre -Emerick Aubameyang,31,wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo.(mirror)
    Hata hivyo, Aubameyang anataka Arsenal kutia saini makubaliano ya hali ya juu kabla ya kukubali mkataba mpya baada ya kuhakikishia klabu hiyo taji ya 14 la kombe la FA. (Le10 sport,via Metro).
    Aston Villa inamlenga mshambuliaji wa Liverpool,25,raia wa Ubelgiji Divock Origi.(Sun).
    Maelezo ya picha
    Troy Deeney alifunga bao lake la 10 katika ligi ya premier msimu huu katika mechi dhidi ya Arsenal
    Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney,32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda.(Mail)
    Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania.(Mundo Deportivo,via talkSPORT)
    Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil,22.(RMC sport, via Express)
    Wakati huohuo United ina matumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling,30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan,25, raia wa Slovakia Milan Skriniar - lakini Roma inaendelea na mchakato wake wa kumtafuta mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo.(Star)
    Mabingwa wa Italia AC Milan na Napoli inafanya mazungumzo na mlinzi wa Uingereza wa timu ya Norwich city,Ben Godfrey,22, baada ya Canaries kushushwa daraja kwenye ligi ya premier. (Calciomercato,via Mail)
    3 min
  • PAPA BENEDICT WA 16 ANA HALI MBAYA.
    Mkuu wa zamani wa kanisa katoliki, Papa Benedict XVl,ameripotiwa kuumwa sana baada ya kumtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa nchini Ujerumani na sasa hali yake ni dhaifu sana.
    Gazeti la Pasaauer Neue presse la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Papa Benedict Mwenye umri wa miaka 93 anasumbuliwa na Ugonjwa unaotokana na kirusi kinachosababisha pelepele usoni na maumivu makali, kwa muujibu wa mwandishi wa tawasifu ya Papa huyo , Peter Seewald.
    Kwa muujibu wa Seewald,"Papa kwa sasa ana hali dhaifu sana" limeandika gazeti hilo ."Akili na uwezo wake wa kufikiri bado viko makini lakini sauti yake inasikika kwa shida sana.
    Seewald alimtembelea Papa Benedict mjini Rome siku ya Jumamosi Agosti 01 kumkabidhi tawasifu yake.
    "Kwenye mkutano huo licha ya kuumwa kwake, Papa alikuwa na matumaini na kusema kwamba endapo hali yake itaimarika, atachukua kalamu tena aandike," limeandika gazeti hilo.
    Papa Benedict alimtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa aitwaye Georg nchini Ujerumani mwezi Juni,ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya Italia tangu alipojiuzulu ghafla upapa mwaka 2013.
    Georg Ratzinger alifariki dunia wiki mbili tu baada ya hapo akiwa na umri wa miaka 96.
    Papa huyo wa zamani, ambaye jina lake halisi ni Joseph Ratzinger,sasa anaishi kwenye nyumba ndogo ya watawa mjini Vatican.
    Tangu awe Papa wa kwanza kujiuzulu kwa takribani miaka 600 iliyopita,amekuwa haonekani sana hadharani kutokana na hali yake ya kiafya.
    Akiwa mwanamapokea ya kanisa katoliki, nafasi yake ilichukuliwa na mwanamgeuzi Papa Francis.
    2 min
  • MAMBO MATATU AMBAYO NI SUMU KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI.
    Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwasababu moja ama nyingine anakuondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa.si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unasababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida.pengine ndio maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la "kudata" kutokana na mapenzi.
    Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama moja wapo ya mambo haya yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza basi fahamu kuwa yamkini unependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi.kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo kwani katika kila jambo kunahitajika kiasi.
    Yafuatayo ndio mambo ambayo ni sumu katika mahusiano ya kimapenzi
    Kumuingilia mpenzi wako katika mambo yake
    Unaweza kujikuta ukisumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini kwa wakati gani, akutane na nani kwa wakati gani au ale nini.ukiona fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.
    Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa kijinsia, hakuna mwanamke angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake, kama ilivyo dokezwa hapo juu kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu.kama unataka kumpangia kila kitu ni wazi utaishia kuishi pekee yako.
    Kutompa nafasi mpenzi wako
    Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumuona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa pekee yake kwaajili ya mambo yake binafsi.
    Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, ila kwa hakika hiyo siyo ishara njema ya mapenzi ya kudumu. hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote.
    Ni wazi kuwa utachoka, kwahiyo mpe mpenzi wako fursa ya kupumua.namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu itaisha.
    Wivu kupindukia
    Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomuona mpenzi wako akizungumza na mwanaume mwingine,au anapotoka na marafiki zake wa kike,au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa unakunywa sumu ya mapenzi.
    Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana.kama kweli unataka Mpenzi yako akupende kwa dhati,mwonyeshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.
    Kama ukizingatia mambo haya machache katika mahusiano yako ya kimapenzi na kama kweli mnapendana na mnamalengo ya kufika mbali na mahusiano yenu basi zingatia haya na utayafurahia mahusiano yenu na yatakuwa mfano wa kuigwa na watu wengine.
    4 min

About Msasa Media

From the publisher's feed

Msasaonline inaamini kila binadamu ana haki ya kuhabarika kuburudika, na kuelimika hivyo basi kazi yetu kuhakikisha tunakuletea habari sahihi, na kupunguza msongo wa mawazo kwa burudani nzuri na…